Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Question to Prime Minister

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 43 Planning and Investment Maswali kwa Waziri Mkuu 6 2026-06-04

Name

Ali Hassan Omar King

Gender

Male

Party

CCM

Constituent

Jang'ombe

Primary Question

MHE. ALI HASSAN OMAR KING: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kupata nafasi hii ya kuuliza swali kwa Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, nchi yetu imekuwa inafanya utaratibu na jitihada mbalimbali katika kukaribisha wawekezaji wa kigeni kwa jitihada kubwa ambazo tunaziona kama vile viongozi wetu kutoka nje ya nchi kufanya mialiko, mabalozi wetu kutumia economic diplomacy, lakini hata jitihada za ndani TISEZA wanazofanya kwa vivutio tofauti, lakini baada ya uwekezaji kunakuja kujitokeza vikwazo vya kikodi, kwa kusema kwamba tunawalinda wawekezaji wa ndani.

Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mkakati gani ambao utafanya kuwawezesha wawekezaji wa ndani bila ya kuweka vikwazo vya kikodi kwa wawekezaji wa nje. Tukiamini kwamba foreign direct investment ina asilimia kubwa sana katika dira yetu katika kukuza uchumi wa nchi yetu? Ninashukuru sana.

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Gender

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa nafasi na nimpongeze Mheshimiwa King, kwa swali zuri.

Mheshimiwa Spika, kumbuka Mheshimiwa King, amekuwa kwenye Kamati ya Bajeti, amekuwa kwenye kamati mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya kiuchumi kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, hoja aliyoitoa Mheshimiwa Mbunge ni ya msingi na kimsingi hivi ndivyo ambavyo Serikali imekuwa ikifanya na tutaendelea kurekebisha kama bado kuna dosari zinajitokeza.

Mheshimiwa Spika, tunahitaji uwekezaji wote, uwekezaji wa ndani na uwekezaji wa nje. Maeneo ambapo kunakuwepo na hoja za kikodi, kimsingi hakulengi sana kwamba ni kwa ajili ya kulinda wawekezaji wa ndani. Maeneo ambayo yanahusisha masuala ya kikodi kumekuwa na vivutio ambavyo wawekezaji wa nje wanapata vingi tu ambavyo wamekuwa wakivipata.

Mheshimiwa Spika, wawekezaji mahiri, wawekezaji mahiri maalumu na wamekuwa wakipewa taratibu za kufuata. Hata hivyo katika siku za hivi karibuni tumeongeza tu maboresho kwamba tusivutie peke yake wawekezaji wa nje, kuna umuhimu wa kuvutia pia wawekezaji wa ndani. Kwa hiyo, na wenyewe tumewawekea utaratibu pamoja na viwango vilevile vya mitaji ambayo zamani ilikuwa inalinganishwa na yule anayetoka nje.

Mheshimiwa Spika, sasa kumekuwa na dirisha mahsusi kwa wawekezaji wa ndani na kumekuwa na viwango maalumu kwa wawekezaji wa ndani ili kuweza kuwafanya wakidhi, tukiwa tumeanza na kiwango cha chini cha dola laki moja, katika sheria ya juzi ile tuliyoitunga ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Uwekezaji. Sasa tumeshusha iwe dola 50,000 kwa wawekezaji wa ndani.

Mheshimiwa Spika, kitu peke ambacho tulikiweka kisheria kinachohusu Watanzania ilikuwa ni kwenye hizi shughuli za uzalishaji, ujenzi na kwingineko. Tuliona kuna umuhimu wa kujenga sekta binafsi ya ndani. Sheria ya zamani ilikuwa inasema, watanzania wanaweza tu wakachukua asilimia kadhaa kwenye mradi, labda 30 au kupitia local content na sheria yenyewe ilikuwa inasema kwamba miradi yote ile lazima ifanywe na wageni.

Mheshimiwa Spika, wageni wengine walikuwa na uwezo sawasawa na Watanzania. Wengine walikuwa hata wanauwezo chini ya Watanzania, lakini walikuwa wanapata sifa tu ya kupewa mradi kwa sababu wao ni wageni. Hii haikuwa imekaa sawa, Mheshimiwa Rais alisema tusiangalie ugeni peke yake, tutengeneze na sisi sekta binafsi ya ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, katika kufanya hivyo kwa sasa Mtanzania na yeye anaweza kuchukua mradi mkubwa na yeye ndiyo akatoa sub-contract kwa wale wageni na kama atahitaji wawe wengi kiasi gani ama utaalamu kiasi gani na anaweza hata akaajiri wataalamu kutoka nje ili kuweza kuhakikisha kwamba na sisi tunakuwa na makampuni ya ndani yanayoweza kufanya shughuli kubwa na yakafanya kwa ufanisi.

Mheshimiwa Spika, tumeona uamuzi huo wa Mheshimiwa Rais katika kazi zilizofanyika za hivi karibuni, madaraja mengi kati ya yale madaraja takribani 81 yaliyojengwa nchi nzima kufuatia uharibifu ule uliojitokeza. Tuna madaraja mengi yamejengwa na tena yamejengwa kwa ubora na yamejengwa na wakandarasi wazawa. Kwa hiyo, hili ndio eneo ambalo tumeliwekea kwenye sheria tukiwa tunalenga kujenga nguvu ya uchumi inayomilikiwa na Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu uwekezaji hilo lipo wazi kwa mtu yeyote kuja kuwekeza na tunaamini kwamba ni jambo ambalo linachangia kwenye uchumi wetu. Hili la kazi za mikataba; ujenzi, miradi ya barabara, ya maji na mingineyo, tulikuwa tunaiepusha nchi kwamba miradi mingine tumechukua fedha za kukopa halafu tunawapa wakandarasi wageni, wanapata supernormal profit (faida na ya juu) na baada ya hapo wanatuachia sisi kama nchi tukishughulikia mikopo ama madeni ambayo tumekopa kutekeleza miradi hiyo, wao wakiwa wameshachukua faida na wakati uwezo wa Watanzania ambao wangeweza kufanya kwa kiwango kilekile upo. Kwa hiyo, hilo ndilo ambalo tumelitofautisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa nafasi. (Makofi)

Additional Question(s) to Prime Minister