Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 7 | Sitting 39 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 343 | 2022-06-07 | 
 
									Name
Selemani Jumanne Zedi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukene
Primary Question
						MHE. SELEMANI J.  ZEDI aliuliza: -
Je, Serikali haioni haja ya kuipandisha hadhi Zahanati ya Kijiji cha Sojo ili kiwe Kituo cha Afya na kuweza kuhudumia wananchi na watumishi wa Mradi wa Bomba la Mafuta?
					
 
									Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
						NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Selemani Jummane Zedi, Mbunge wa Jimbo la Bukene kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Kijiji cha Sojo ni moja kati ya vijiji saba vya Kata ya Igusule yenye wakazi 23,237. Kata hii ina zahanati moja iliyopo katika Kijiji   cha Sojo ambayo inaendelea kutoa huduma kwa wananchi.
Mheshimiwa Spika, Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023 imetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya kwenye Kata ya  Igusule.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved