Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 14 | Sitting 5 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 72 | 2024-02-05 | 
 
									Name
Masache Njelu Kasaka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lupa
Primary Question
						MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Makongolosi – Rungwa?
					
 
									Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
						NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Masache Njelu Kasaka, Mbunge wa Lupa, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Mbeya – Chunya – Makongolosi – Rungwa – Mkiwa (kilometa 503.36) kwa awamu; ambapo sehemu ya Mbeya – Chunya – Makongolosi (kilometa 111) ujenzi umekamilika.  Ujenzi wa sehemu ya Noranga – Itigi – Mkiwa (kilometa 56.9) sehemu ya Noranga – Itigi (kilometa 25.) umefikia asilimia 72 na kwa sehemu ya Noranga – Doroto (kilometa 6) na Itigi – Mkiwa (kilometa 25.6) kazi ya ujenzi imeanza na utekelezaji wa mradi unaendelea.  Kwa sehemu iliyobaki ya barabara ya Makongolosi – Rungwa – Noranga (kilometa 356) Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi, ahsante.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved