Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 15 | Sitting 22 | Energy and Minerals | Wizara ya Madini | 292 | 2024-05-09 | 
 
									Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
						MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: - 
Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilaya ya Ulanga?
					
 
									Name
Anthony Peter Mavunde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Dodoma mjini
Answer
						WAZIRI WA MADINI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali ni kuwasaidia wachimbaji wadogo nchini wakiwemo wachimbaji wa madini wa Wilaya ya Ulanga unahusisha mambo yafuatayo:-
(i)	Kuwekeza zaidi katika utafiti wa kina kugundua uwepo wa madini katika maeneo mbalimbali ili kuwaongoza vizuri wachimbaji wadogo;
(ii)	Utoaji wa Leseni za uchimbaji kwa wachimbaji wadogo;
(iii)	Kutoa elimu ya matumzi ya teknolojia sahihi ya uchimbaji ili kuongeza tija;
(iv)	Huduma ya uchorongaji kwa gharama nafuu kupitia Shirika la Madini Tanzania (STAMICO); 
(v)	 Upatikanaji wa mikopo nafuu kwa wachimbaji; na
(vi)	Fursa ya ukodishaji wa mitambo na vifaa chini ya usimamizi wa STAMICO. 
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved