Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 15 | Sitting 25 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 331 | 2024-05-14 | 
 
									Name
Hassan Zidadu Kungu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kaskazini
Primary Question
						MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza:-
Je, lini Serikali itakamilisha uchimbaji wa visima vya maji vilivyoanza kuchimbwa katika Jimbo la Tunduru Kaskazini?
					
 
									Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
						NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hassan Zidadu Kungu, Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilipanga uchimbaji wa visima 13 katika Wilaya ya Tunduru, hususan katika Jimbo la Tunduru Kaskazini. Hadi sasa visima vitatu vimechimbwa katika Vijiji vya Fundimbanga, Ligunga na Majala. Aidha, taratibu za uchimbaji wa visima 10 katika Vijiji vya Ngapa, Mkanyageni, Malombe, Mkapunda, Namiungo, Sisi-kwa-Sisi, Mtengashari, Tumaini, Mkwajuni na Msamala zinaendelea ambapo uchimbaji wa visima hivyo unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2024.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved