Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 12 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 128 | 2026-04-20 |
Name
Sheila Edward Lukuba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHEILA E. LUKUBA aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga mfereji mkubwa kuelekeza maji Mto Ngerengere ili kunusuru Wakazi wa Kata ya Kihonda na Lukobe kwa mafuriko?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Sheila Edward Lukuba, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata za Kihonda na Lukobe katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro zimekuwa zikiathiriwa na mafuriko ya mara kwa mara nyakati za mvua. Ili kutatua changamoto hiyo, Serikali imepanga kujenga mifereji ili kuyaelekeza maji katika Mto Ngerengere. Serikali imeunda timu ya wataalam kwa ajili ya kufanya tathmini na kuandaa andiko la mradi ambalo litaonesha mahitaji halisi na njia nzuri ya kulifanyia kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, timu ya tathmini inatarajia kukamilisha kazi hiyo kabla au ifikapo Septemba, 2026. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved