Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 39 | Youth, Disabled, Labor and Employment | Ofisi ya Rais: Maendeleo ya Vijana | 461 | 2026-05-29 |
Name
Latifa Khamis Juwakali
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SYLVIA F. SIGULA K.n.y. MHE. LATIFA KHAMIS JUWAKALI aliuliza: -
Je, Serikali imejipangaje kuwafikia vijana wenye ujuzi na kuwapatia mafunzo ya ziada na mikopo?
Name
Joel Arthur Nanauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtwara Mjini
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MAENDELEO YA VIJANA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Latifa Khamis Juwakali, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kuwafikia vijana wenye ujuzi ili kuwaongezea uwezo wa kitaalamu, kuwajengea mazingira ya kujiajiri na kuwawezesha kupata mikopo kwa ajili ya shughuli za uzalishaji na maendeleo ya kiuchumi. Kupitia programu za uwezeshaji wa vijana zinazotekelezwa na Wizara za Kisekta, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano pamoja na Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Serikali inaendelea kutoa mafunzo ya ujasiriamali, ubunifu, matumizi ya teknolojia na stadi za kazi kulingana na mahitaji ya soko la ajira. Aidha, vijana wanaendelea kunufaika na mikopo yenye masharti nafuu kupitia programu na mifuko ya uwezeshaji wa vijana ikiwemo 10% ya mapato ya halmashauri zinazotengwa kwa ajili ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali pia imeendelea kuimarisha ushirikiano na taasisi za elimu na mafunzo ya ufundi pamoja na sekta binafsi ili kuwafikia vijana wengi zaidi wenye ujuzi nchini kupitia utambuzi wa vikundi vya vijana, usajili wa miradi yao na utoaji wa elimu ya fedha na usimamizi wa biashara. Kupitia hayo yote Serikali inalenga kuongeza uwezo wa vijana kujitegemea kiuchumi, kuongeza ajira na kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved