Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 39 | Youth, Disabled, Labor and Employment | Ofisi ya Rais: Maendeleo ya Vijana | 462 | 2026-05-29 |
Name
Cecilia Daniel Paresso
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza: -
Je, lini wanawake wajasiriamali wa Mkoa wa Arusha watafikiwa na fursa ya mkopo wa shilingi bilioni 200 uliotolewa na Mheshimiwa Rais?
Name
Joel Arthur Nanauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtwara Mjini
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MAENDELEO YA VIJANA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cecilia Daniel Paresso, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua mchango mkubwa wa wanawake katika kukuza uchumi na maendeleo ya Taifa. Kupitia shilingi bilioni 200 zilizotolewa na Mheshimiwa Rais kwa ajili ya mikopo yenye masharti nafuu kwa makundi mbalimbali, wanawake wakiwemo wa Mkoa wa Arusha wamepewa wigo mpana wa kunufaika na fursa hiyo. Mbali na fedha zinazotengwa kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, wanawake pia wanaendelea kunufaika kupitia mifuko na programu za Wizara nyingine za kisekta, pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana katika Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika awamu ya kwanza ya utekelezaji, wanawake vijana 147 wa Mkoa wa Arusha wanatarajiwa kunufaika na mikopo hiyo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana itakayotolewa mwanzoni mwa mwezi Juni, 2026. Aidha, Serikali itaendelea kuhakikisha kuwa wanawake wengi zaidi wanapata fursa hizi kupitia mifumo na taratibu zilizowekwa, kwa lengo la kuongeza ushiriki wao katika shughuli za uzalishaji na kukuza uchumi wa Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved