Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2015-2020 | Session 18 | Sitting 4 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 38 | 2020-01-31 | 
 
									Name
Sixtus Raphael Mapunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Mjini
Primary Question
						MHE. MARIAM N. KISANGI (K.n.y. MHE. SIXTUS R. MAPUNDA) aliuliza:-
Tangu mwaka 2016, Serikali iliahidi kuboresha huduma za afya katika Hospitali ya Wilaya ya Mbinga ikiwa ni pamoja na kujenga wodi ya watoto, chumba cha upasuaji na gari la wagonjwa:-
Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi hizo?
					
 
									Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Answer
						NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, nakushukuru, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sixtus Raphael Mapunda, Mbunge wa Mbinga Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya Hospitali ya Halmashauri ya Mji Mbinga ambapo kupitia mapato yake ya ndani Halmashauri ya Mji Mbinga imefanya ukarabati wa jengo  la „Grade A‟  kwa gharama ya  Shilingi  milioni  45  na  kununua jokofu la kuhifadhia maiti lenye thamani ya Shilingi milioni 29.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imetoa kiasi cha Shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kalembo ili kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Mbinga, ahsante.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved