Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2015-2020 | Session 18 | Sitting 5 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 62 | 2020-02-03 | 
 
									Name
Oran Manase Njeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbeya Vijijini
Primary Question
						MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza:-
Halmashauri ya Mbeya ina upungufu mkubwa wa maji karibu kwenye Vijiji zaidi ya 153 na   hasa   katika   Kata   ya   Mjele.    Je,    Serikali    ina    mpango    gani    wakupeleka maji    kwenye Vijiji hivyo na hasa Vijiji vya Mjele, Chang‟ombe na Ipwizi?
					
 
									Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
						NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Oran Manase Njenza, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua tatizo la maji lililopo katika Halmashauri ya Mbeya Vijijini, katika mwaka wa fedha wa 2019/2020, Serikali imepanga kutekeleza miradi tisa ya maji ambayo  ni  Idimi - Haporoto,  Iwindi,  Mshewe,  Ipwizi,   Mjele - Chang‟ombe, Galijembe, Nsenga - Wimba, Iyawaya na Isangala group . Kiasi cha shilingi bilioni 6.4 kimetengwa katika bajeti ya 2019/20 kwa ajili ya kazi hiyo.  Hadi kufikia mwezi Disemba 2019,   jumla   ya   miradi   2 ya Idimi - Haporoto na Iwindi imekamilika na kiasi cha fedha shilingi bilioni 1.5 kimetumika katika ujenzi wa miundombinu ya maji.
Mheshimiwa   Spika,   baada   ya   Serikali    kukamilisha    miradi    yote    iliyopo kwenye  bajeti  ya   2019/2020,   jumla   ya   vijiji   21   vitapata    huduma    ya    maji vikiwemo vijiji vya Mjele, Chang‟ombe na Ipwizi ambapo jumla ya wakazi wapatao 44,364 watanufaika.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved