Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2015-2020 | Session 18 | Sitting 6 | Finance and Planning | Wizara ya Fedha na Mipango | 80 | 2020-02-04 | 
 
									Name
Juma Selemani Nkamia
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chemba
Primary Question
						MHE. JUMA S. NKAMIA ali uliza:-
Je, Serikali imekusanya kiasi gani cha kodi kutoka kwa makocha na wachezaji wa kigeni wanaofanya kazi nchini katika mwaka wa fedha 2017/2018?
					
 
									Name
Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Kondoa
Answer
						NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO alijibu:-
Mheshimiwa   Mwenyekiti,    kwa     niaba     ya     Waziri     wa     Fedha     na Mipango, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Juma Suleimani Nkamia, Mbunge wa Chemba, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti,   kwa   mujibu   wa    Sheria    ya    Kodi    ya    Mapato ya   Mwaka   2004, Kifungu cha 7; “kila mtu anayepata mapato yatokanayo na ajira ndani ya Jamhuri ya  Muungano  wa  Tanzania  anawajibika  kulipa  kodi  ya   mapato kulingana    na    kipato chake.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka 2017/2018, jumla ya shilingi milioni 1,733.6 zilikusanywa kama malipo ya kodi ya ajira kutoka kwa makocha na wachezaji wa kigeni wanaofanya kazi hapa nchini.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved