Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2015-2020 | Session 18 | Sitting 8 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 97 | 2020-02-06 | 
 
									Name
Willy Qulwi Qambalo
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Karatu
Primary Question
						MHE. WILLY Q. QAMBALO aliuliza:-
Mabaraza ya Ardhi ya Kata ni chombo muhimu sana katika kutatua migogoro ya ardhi. Hata hivyo, changamoto kubwa ni uwezeshaji (chakula na nauli) na wajumbe wa mabaraza hayo ili wafanye kazi zao kwa weledi. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha wajumbe wanawezeshwa ili waweze kutoa haki?
					
 
									Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Answer
						NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Qambalo Willy Qulwi, Mbunge wa Karatu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Kifungu cha 7 cha Sheria ya Mabaraza ya Ardhi ya Kata kinazipa Halmashauri wajibu wa kutengeneza utaratibu wa namna ya kuwezesha Mabaraza ya Ardhi  na  Kata  kiutendaji  na  kuweka  mazingira  mazuri  ya  kufanyia  kazi.  Mikoa  na  Wilaya imeelekezwa kuzisimamia Halmashauri kuhakikisha Mabaraza hayo yanawezeshwa ili yaweze kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu. Kila Halmashauri inatakiwa kutenga bajeti kila mwaka kwa ajili ya kuhudumia Mabaraza ya Ardhi ya Kata. Ofisi ya Rais, TAMISEMI inaendelea kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji ili kuhakikisha changamoto hiyo inapatiwa ufumbuzi, ahsante.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved