Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 9 | Sitting 2 | Health and Social Welfare | Wizara ya Afya | 26 | 2022-11-02 | 
 
									Name
Abdulhafar Idrissa Juma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtoni
Primary Question
						MHE. IDRISSA JUMA ABDUL-HAFAR aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kupambana na visababishi vya maradhi yasiyoambukiza?
					
 
									Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
						NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Afya, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Idrissa Juma Abdul-Hafar, Mbunge wa Jimbo la Mtoni, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga shilingi milioni 725 kwa ajili ya kutekeleza Mpango Mkakati wa Tatu wa Kitaifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza (2021 – 2026) ambao umeainisha mikakati mahsusi ya udhibiti wa visababishi vya magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo:-
(1)	Kuimarisha uratibu na ushirikishwaji wa sekta mtambuka;
(2)	Kuimarisha miundombinu ya utoaji wa huduma; 
(3)	Kuwajengea uwezo watumishi katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza; 
(4)	Kuimarisha na kusimamia shughuli za utafiti; na 
(5)	Kuhamasisha wananchi kuhusu njia za kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza. 
Njia hizi ni pamoja na kufanya mazoezi, pamoja na kuzingatia kanuni bora za lishe.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved