Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 10 | Sitting 4 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 64 | 2023-02-03 | 
 
									Name
Aloyce John Kamamba
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kakonko
Primary Question
						MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza: -
Je, lini minara ya mawasiliano itapelekwa Kata za Nyamtukuza, Nyabibuye, Gwarama, Kasuga, Rugenge, Gwanumpu, Katanga na Magunzu?
					
 
									Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
						NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI, alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Aloyce John Kamamba, Mbunge wa Buyungu, kama ifuatavyo: -
 
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya Vodacom imetekeleza miradi ya kufikisha huduma za mawasiliano ya simu katika Kata za Nyamtukuza, Nyabibuye, Gwarama, Gwanumpu, Rugenge na Mugunzu. Miradi hii imetekelezwa kati ya mwaka 2016 na 2019 ambapo ujenzi wa minara katika Kata hizi umekamilika na inatoa huduma kwa teknolojia ya 2G na 3G.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Kata ya Katanga na Kasuga, Serikali itafanya tathmini ya hali halisi ya upatikanaji wa huduma za mawasiliano Kata hizi katika mwaka wa fedha 2023/2024, ahsante.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved