Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 10 | Sitting 5 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 72 | 2023-02-06 | 
 
									Name
Yustina Arcadius Rahhi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
						MHE. YUSTINA A. RAHHI aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kiwanja cha Ndege katika Mkoa wa Manyara?
					
 
									Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
						NAIBU WAZIRI	WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yustina Arcadius Rahhi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea  na utaratibu wa kutwaa eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Mkoa wa Manyara.
Mheshmiwa Mwenyekiti, hadi sasa Serikali imeshamaliza kuandaa hadidu za rejea kwa ajili ya kumpata mhandisi elekezi atakayefanya upembuzi yakinifu pamoja na usanifu wa kina ili kubaini gharama za ujenzi. Hivyo, ujenzi wa kiwanja hicho utaanza baada ya usanifu kukamilika, ahsante.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved