Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 10 | Sitting 8 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 128 | 2023-02-09 | 
 
									Name
Subira Khamis Mgalu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
						MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa kiwango cha lami kwa barabara ya Mziha – Kibindu – Mbwewe?
					
 
									Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Answer
						NAIBU WAZIRI	WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE) alijibu: -
 
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Subira Khamis Mgalu, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kabla ya kuanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, kunahitajika kufanyika upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara ya Mziha – Kibindu – Mbwewe yenye urefu wa kilometa 68.63. Baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na gharama za ujenzi kujulikana Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi huu, ahsante.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved