Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 12 | Sitting 3 | Enviroment | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 42 | 2023-08-31 | 
 
									Name
Joseph Anania Tadayo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwanga
Primary Question
						MHE. JOSEPH A.  TADAYO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itatekeleza mradi wa kuondoa magugu maji katika Ziwa Jipe?
					
 
									Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Answer
						WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Anania Tadayo, Mbunge wa Mwanga kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ofisi imeona changamoto ya uharibifu wa mazingira unaotokana na kuenea kwa magugu maji katika Ziwa Jipe. Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira tayari imefanya tathimini ya uharibifu uliopo na  kuandaa andiko la mradi  wa hifadhi ya ardhi, na vyanzo vya maji wenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni sita  kwa ajili ya kuondoa magugu maji katika Ziwa Jipe ambapo hadi sasa jitihada za kutafuta fedha kutoka kwa wafadhili mbalimbali zinaendelea. 
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni nia ya Serikali kuhakikisha inarejesha ikolojia ya Ziwa Jipe ili kuleta manufaa kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo pamoja na uhifadhi wa mazingira. Serikali inamhakikishia Mbunge kwamba mara fedha zitakapopatikana  itatekeleza mradi huu mara moja. Ahsante sana.
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved