Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date | 
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 11 | Sitting 42 | Health and Social Welfare | Wizara ya Afya | 554 | 2023-06-07 | 
 
									Name
Bernadeta Kasabago Mushashu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
						MHE. BENARDETA K. MUSHASHU aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti Magonjwa yasiyoambukiza?
					
 
									Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
						NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Afya, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bernadeta Kasabago Mushashu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- 
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/2023, Serikali imetenga shilingi milioni 725 kwa ajili ya kutekeleza Mpango Mkakati wa Tatu wa Kitaifa wa Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza (2021 – 2026) ambapo umeainisha mikakati mahususi ya udhibiti wa visababishi vya magonjwa yasiyoambukiza ambayo ni kuimarisha uratibu na ushirikishwaji wa sekta  mtambuka; Kuimarisha miundombinu ya utoaji wa huduma; Kuwajengea uwezo watumishi katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza; Kuimarisha na kusimamia shughuli za utafiti; pamoja na kuhamasisha wananchi kuhusu njia za kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza. Njia hizi ni kufanya mazoezi, pamoja na kuzingatia kanuni bora za lishe.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha. 
					
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved