Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. AZIZA S. ALLY aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa maboma ya zahanati na shule yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi Nzega?

Supplementary Question 1

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri kabisa ya Serikali, nina swali moja tu la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa maboma haya mengi yana muda mrefu sana, Serikali haioni umuhimu sasa wa kufanya tathmini ya kina na kuweza kubaini maboma yote nchi nzima ili iweze kutenga bajeti kwa wakati mmoja na kumaliza changamoto ya umaliziaji wa haya maboma? Ahsante. (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba wananchi wameitikia wito wa Serikali na kuchangia nguvu zao kwa ajili ya ujenzi wa maboma ya zahanati na madarasa na tayari Serikali ilishafanya tathmini na kuyatambua na kuyaorodhesha maboma yote ya zahanati na madarasa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi na kila mwaka wa fedha Serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kwenda kuyakamilisha maboma hayo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu ili kukamilisha maboma ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi. Ahsante sana.

Name

Yahaya Omary Massare

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Magharibi

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. AZIZA S. ALLY aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa maboma ya zahanati na shule yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi Nzega?

Supplementary Question 2

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, katika Halmashauri ya Itigi yapo maboma mengi ya shule katika kata karibu zote, lakini na maboma ya zahanati. Je, Serikali ipo tayari sasa kupeleka fedha katika Halmashauri ya Itigi kumalizia maboma haya ambayo wananchi walijitolea? Ahsante sana.

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali ipo tayari kupeleka fedha kwa ajili ya kumalizia maboma ya zahanati na madarasa katika Halmashauri ya Itigi na imekuwa ikifanya hivyo kila mwaka wa fedha na zahanati kadhaa zimekamilishwa, lakini madarasa yamekamilishwa. Nimhakikishie Mheshimiwa Massare kwamba tutaendelea kuweka kwenye bajeti ya kila mwaka ili kukamilisha maboma hayo ya zahanati na shule katika Halmashauri ya Itigi. Ahsante.