Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza:- Je, lini Serikali italitengeneza na kulitangaza Daraja la Mungu la kihistoria lililopo Wilaya ya Rungwe ambalo lipo katika hali ya kutotunzwa?
Supplementary Question 1
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, ninaishuruku Serikali kwa majibu mazuri ambayo imeyatoa, lakini hukohuko Rungwe kuna daraja lingine ambalo linaunganisha Makete na Rungwe, kwa maana ya Kata ya Kigulu na Kata nyingine ya Mbigili. Je, ni lini Serikali itajenga daraja hilo ambalo kwa kweli linatumika na wananchi wengi na hadi sasa niseme wazi hicho Kijiji cha Kigulu hakijawahi kuona hata gari, lakini wanategemea daraja hilo lijengwe, ni yapi maelekezo ya Serikali hasahasa kwenye ule mradi ambao umekuwa ukisaidia maeneo kama haya?
 
											Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ni kweli kwamba kuna daraja ambalo linaunganisha Halmashauri ya Wilaya ya Makete Mkoani Njombe na Halmashauri ya Rungwe Mkoani Mbeya na ni daraja la muhimu sana kwa wananchi wa Wilaya ya Makete na Wilaya ya Rungwe. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ilikwishalitambua hitaji la daraja katika eneo hilo na tunaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kwenda kujenga daraja lile ili wananchi wa Rungwe na wa Makete na Mikoa ya Njombe na Mbeya ipate mawasiliano ya uhakika zaidi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved