Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Agnes Elias Hokororo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AGNES E. HOKORORO K.n.y. MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:- Je, lini Serikali itatatua changamoto ya uhaba wa Walimu katika Halmashauri ya Mji Nanyamba?

Supplementary Question 1

MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, ninaomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; baadhi ya Halmashauri za miji kama Nanyamba, Newala na Masasi zina mwonekano wa vijijini kibajeti, kwa maana ya kuwa na bajeti ndogo; je, Serikali haioni ipo haja ya kuweka mgao sawa wa walimu katika halmashauri hizo changa au mpya?

Mheshimiwa Spika, …

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri keti kwanza, Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya. Mheshimiwa Agnes Hokororo swali la pili.

MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Spika, Shule ya Sekondari Dinyecha ina wanafunzi zaidi ya 818; kwa kidato cha tano na cha sita, ni wasichana lakini ina upungufu mkubwa sana wa walimu wa sayansi. Je, Serikali ina mkakati gani wa dharura wa kuwaokoa hawa wasichana kwa sababu pia kuna mkakati wa kuwafanya wasichana wasome sayansi? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Halmashauri za Miji Nanyamba, Masasi na halmashauri nyingine zote kote nchini zinapewa watumishi wa Sekta ya Elimu kwa maana ya walimu kwa kuzingatia upungufu ya idadi ya walimu waliopo katika halmashauri hizo na si kwa kuzingatia hadhi kwamba ni halmashauri za mji. Kwa hivyo, katika utaratibu wetu wa ajira tumeweka makundi matatu: kundi la kwanza ni mikoa na halmashauri zenye upungufu mkubwa zaidi wa walimu; lakini kundi la pili ni upungufu wa wastani; na kundi la tatu ni zile halmashauri na mikoa yenye upungufu mdogo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kuwa halmashauri ya Mji haiathiri ikama ya watumishi wanaopelekwa kwa sababu kigezo ni kujua watumishi wangapi wanahitajika, wangapi wapo na hivyo tunapeleka kwa kipaumbele kwenye halmashauri zile zenye upungufu mkubwa ikiwemo Nanyamba, Masasi na halmashauri nyingine kote nchini.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na Shule ya Sekondari Dinyecha ambayo ina upungufu mkubwa wa walimu wa sekondari kwa maana ya walimu wa sayansi, ninaomba nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba katika ajira za Sekta ya Elimu, Serikali imeweka kipaumbele kikubwa zaidi kwa walimu wa sayansi na walimu hao wamekuwa wakiajiriwa na kupelekwa kwenye shule zote zenye upungufu mkubwa zaidi wa walimu hao wa sayansi. Kwa hivyo, tutahakikisha pia shule ya Sekondari Dinyecha tunaitazama kwa jicho la karibu ili iweze kupata waalimu hao na kuboresha huduma za elimu.

Name

Shamsia Aziz Mtamba

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Mtwara Vijijini

Primary Question

MHE. AGNES E. HOKORORO K.n.y. MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:- Je, lini Serikali itatatua changamoto ya uhaba wa Walimu katika Halmashauri ya Mji Nanyamba?

Supplementary Question 2

MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kwa kunipatia nafasi ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Tatizo lililopo Nanyamba linafanana kabisa na tatizo lililopo katika Jimbo la Mtwara Vijijini. Je, ni lini Serikali itatatua changamoto ya uhaba wa walimu katika Jimbo la Mtwara Vijijini? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Mtwara na Halmashauri zake zote ni moja ya mikoa 10 ambayo tumeitambua kwamba ni mikoa yenye upungufu mkubwa zaidi wa watumishi wa sekta zote ikiwemo Sekta ya Elimu; ikiwemo Halmashauri ya Mtwara Vijijini. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Shamsia kwamba Halmashauri yake ni moja ya halmashauri ambazo zimewekewa kipaumbele na kwenye kila ajira za kila mwaka tumekuwa tukipeleka watumishi wengi zaidi na tunaendelea kufanya hivyo ili kuweza kupunguza pengo la walimu katika halmashauri hiyo. Ahsante.