Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Esther Lukago Midimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER L. MIDIMU K.n.y. MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani kujenga miundombinu ya maji shuleni ili kuepuka milipuko ya magonjwa?

Supplementary Question 1

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini sasa Serikali itapeleka hiyo miundombinu ya maji katika shule zilizobaki? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na zoezi hili ni endelevu la kuboresha miundombinu ya maji katika shule zetu katika Mkoa wa Simiyu na katika mikoa yote kote nchini. Kwa hivyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge wote kwamba tutaendelea katika kila bajeti ya mwaka kutenga fedha kutoka vyanzo mbalimbali kwa ajili ya kuboresha huduma za maji katika shule zetu. (Makofi)

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER L. MIDIMU K.n.y. MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani kujenga miundombinu ya maji shuleni ili kuepuka milipuko ya magonjwa?

Supplementary Question 2

MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba shule zinazojengwa sasa zinawekewa miundombinu ya uvunaji wa maji ya mvua ili kuzisaidia ziweze kupata maji safi na salama? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Mkakati wa Serikali ni kwamba tumetoa maelekezo na mwongozo rasmi kwamba shule zote zinazojengwa, lakini pia vituo vya huduma za afya lazima kwanza viwe na miundombinu ya kuvuna maji ya mvua ikiwemo kufunga gata kwenye majengo yote, lakini kuchimba visima kwa ajili ya kuhifadhi maji ya mvua. Kwa hiyo, zoezi hilo linafanyika na shule zote, kwa mfano za mikoa 26 za wasichana zote zina miundombinu hiyo mahususi kwa ajili ya kuvuna maji, lakini shule ambazo zimejegwa hivi sasa za SEQUIP zimeendelea pia kuwekewa miundombinu ya maji. Zoezi hili ni endelevu, tutaendelea kulisimamia kuhakikisha watoto wetu wanapata maji ya uhakika katika shule zao. Ahsante sana.