Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Khamis Yussuf Mussa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwahani

Primary Question

MHE. KHAMIS YUSSUF MUSSA aliuliza:- Je, lini Serikali itainufaisha Zanzibar katika matumizi ya nishati ya gesi kutumika katika magari?

Supplementary Question 1

MHE. KHAMIS YUSSUF MUSSA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Pamoja na majibu hayo mazuri nina swali moja la nyongeza pamoja na ushauri.

Mheshimiwa Spika, swali langu lipo hivi, je, Serikali imejipangaje katika kutoa elimu juu ya matumizi ya gesi katika magari Visiwani Zanzibar?

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu ni kwamba mafunzo yatakapotolewa yawalenge hasa watumishi wa Serikali pamoja na Wizara na Mashirika ili wao ndiyo wawe changamoto kubwa sana katika kuwashajihisha watumiaji wengine binafsi.

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa swali la Mheshimiwa Mbunge. Kama ambavyo nimetangulia kusema tutaendelea kushirikiana na wenzetu wa ZPDC kwa sababu tayari tuna ushirikiano basi na hilo la lenyewe tutalichukua kwa ajili ya kufanya kazi kwa pamoja na wao waweze kulichukua na kulifanyia kazi kwa upande wa Zanzibar. (Makofi)