Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Yahaya Omary Massare
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Magharibi
Primary Question
MHE. YAHAYA O. MASSARE K.n.y. MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:- Je, nini mpango wa kuhakikisha Vijiji vya Mkalama vilivyopo umbali wa Kilometa 20 litakapopita Bomba la Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria vinapata maji?
Supplementary Question 1
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri sana ambayo yanatia matumaini kwa wananchi wa Mkoa wa Singida, lakini na Mkoa wa Dodoma, nina swali moja tu la nyongeza. Je, Serikali sasa iko tayari wakati inafanya upembuzi yakinifu kuhusisha Mji wa Itigi katika Mradi huu wa Maji wa Ziwa Victoria wakati unakuja Dodoma kutokea Singida?
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua uhitaji wa maji kwa wananchi wake wote na ipo tayari kufanya hivyo Itigi na maeneo mengine ya Mikoa ya Singida na Dodoma. Ahsante sana. (Makofi)
 
											Name
Hussein Nassor Amar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyang'hwale
Primary Question
MHE. YAHAYA O. MASSARE K.n.y. MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:- Je, nini mpango wa kuhakikisha Vijiji vya Mkalama vilivyopo umbali wa Kilometa 20 litakapopita Bomba la Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria vinapata maji?
Supplementary Question 2
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itaanza kufunga mita za prepaid kwa Mkoa wa Geita na Wilaya yake ya Nyang’hwale? Ahsante. (Makofi)
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, Serikali kwa utaratibu wake na kwa maelekezo ya Mheshimiwa Rais, tayari tumeshaanza kufunga prepaid water meter katika maeneo mengine. Pia ni maelekezo ya Serikali kuendelea kufunga mita ili kuendelea kuondoa malalamiko ya bill ambazo wananchi wanadhani kwamba kwa namna moja au nyingine siyo bill halisi kwa ajili ya matumizi yao. Kwa hiyo, yako maelekezo mahsusi kwa Mkoa wa Geita pamoja na Wilaya ya Nyang’hwale pia ya kuhakikisha kwamba tunafunga prepaid water meter. Ahsante sana.
 
											Name
Boniphace Nyangindu Butondo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kishapu
Primary Question
MHE. YAHAYA O. MASSARE K.n.y. MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:- Je, nini mpango wa kuhakikisha Vijiji vya Mkalama vilivyopo umbali wa Kilometa 20 litakapopita Bomba la Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria vinapata maji?
Supplementary Question 3
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Bomba hili litakalokuwa linasafirisha maji kutoka Ziwa Victoria litakuwa linapitia Ihelele huko Mwanza. Pia, litakuwa linapitia katika wilaya ya jirani kabisa ambayo ni Kishapu, Kata ya Busangwa, Kata ya Mondo, Kata ya Sekebugolo na Kata ya Bubiki; ambazo ni kata zilizomo ndani ya kilometa 12…
SPIKA: Mheshimiwa Butondo, ni swali la nyongeza. Ni swali la nyongeza. 
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Spika, Serikali inasema nini juu ya hatua ya utelekelezaji wa mradi huu kunufaisha wananchi wa Kishapu? (Makofi)    
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa kama ifuatavyo:- 
Mheshimiwa Spika, ninafahamu kiu ya Mheshimiwa Butondo kwa wananchi wake wa Kishapu na Serikali tunatambua kiu hiyo kwa sababu ndiyo dhamira ya Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kuhakikisha watu wake wanapata huduma ya maji safi na salama. Hivyo, nimtoe wasiwasi, Serikali itahakikisha katika upembuzi yakinifu tunaangalia namna bora ya kuhakikisha kwamba tunawafikishia maji, lakini kwa gharama ambayo haitakuwa na changamoto.  Ahsante sana. (Makofi)   
							
 
											Name
Shabani Omari Shekilindi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Primary Question
MHE. YAHAYA O. MASSARE K.n.y. MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:- Je, nini mpango wa kuhakikisha Vijiji vya Mkalama vilivyopo umbali wa Kilometa 20 litakapopita Bomba la Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria vinapata maji?
Supplementary Question 4
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru na ninaishukuru Serikali imetupa shilingi 1,800,000,000 kwa ajili ya kujenga mradi wa maji, lakini ule mradi wa maji, bomba zake zimechomwa moto na mtu na mtu huyo aliyezichoma moto anajulikana. Je, ni nini kauli ya Serikali kwa watu wanaohujumu miundombinu ya maji kwa makusudi? (Makofi)
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, kwanza, ninasikitika kwamba hili ni kosa kama makosa mengine ambapo huyo mtu anatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria na sisi kama Wizara ya Maji na Serikali hatutosita kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria ambayo inaongoza maeneo hayo kwa watu wote wanaohujumu miundombinu, huduma zetu na hata michakato ya ujenzi wa huduma za maji kwa wananchi wetu. Ahsante sana.
 
											Name
Kasalali Emmanuel Mageni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sumve
Primary Question
MHE. YAHAYA O. MASSARE K.n.y. MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:- Je, nini mpango wa kuhakikisha Vijiji vya Mkalama vilivyopo umbali wa Kilometa 20 litakapopita Bomba la Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria vinapata maji?
Supplementary Question 5
MHE. KASALALI E. MAGENI: Mheshimiwa Spika, Mradi wa Kupeleka Maji ya Bomba kutoka Ziwa Victoria katika Jimbo la Sumve kupitia Kata ya Mantale na Malya umekuwa ukisuasua kutokana na malipo kucheleweshwa kwa mkandarasi. Je, Serikali haioni umuhimu wa kumlipa kwa wakati mkandarasi huyu ili mradi huu ukamilike kwa muda kama ilivyopangwa? Ninashukuru.
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, Serikali tunatambua uhitaji wa wakandarasi wetu kulipwa ili kuendelea kutekeleza miradi hii ili iweze kukamilika kwa wakati na iweze kutoa huduma ya maji ambayo imetarajiwa. Pia, ninatambua kwamba Mheshimiwa Mageni amekuwa akiupigania sana Mradi huu wa Ziwa Victoria kwa upande wa Sumve – Mantale na sisi tulishapokea hati za madai na tayari tumeshapeleka Wizara ya Fedha kwa ajili ya malipo ili mkandarasi aweze kuharakisha utekelezaji wa mradi huo. Ahsante sana.