Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Ichenjezya, Hasamba, Nwansana, Vwawa hadi Ilolo utakamilika na kuanza kutoa maji ya uhakika?
Supplementary Question 1
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Spika, kwanza, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. 
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; kwa kuwa, wakandarasi wote wawili wa Mwansyana hadi Vwawa na wa Ichenjezya hadi Vwawa kwa muda mrefu walikuwa wameshaondoka site na wameacha kutekeleza ule mradi. Ni nini kauli ya Serikali kuhakikisha kwamba hawa wakandarasi wanarudi kazini ili waweze kutekeleza mradi huo? (Makofi)
   
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa, tulikubaliana na Serikali suluhu ya muda mrefu na Serikali ikatoa fedha zaidi ya shilingi bilioni saba, ni kuleta mradi wa maji kutoka Mafumbo kuja kuungana na huu mradi ili kuweza kutatua tatizo la maji. Ni lini Mradi huu wa Maji wa Mafumbo utakamilika? (Makofi)         
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Hasunga na kwa kazi nzuri ambayo anaendelea kuifanya katika jimbo lake; kwa hakika amekuwa mwakilishi mwema na ni kweli anafanya kazi.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa wakandarasi ambao wameondoka site, Mheshimiwa Waziri wa Maji, Mheshimiwa Jumaa Hamidu Aweso alimwelekeza Mheshimiwa Katibu Mkuu Engineer Mwajuma Waziri, kuhakikisha anakaa na hao wakandarasi na kuangalia namna bora zaidi ya kwenda kuhakikisha kwamba jambo hili linatatuliwa; hata kama wana madai basi madai hayo yatawafuata wakati wakiwa wanaendelea na utekelezaji wa miradi hiyo kwa sababu tunatambua umuhimu mkubwa wa miradi hii kukamilika ili iweze kuwasaidia wananchi. 
Mheshimiwa Spika, vilevile, kwa upande wa swali la pili, Mradi wa Mafumbo ni mradi wa kimkakati na ni mradi ambao unakuja kuleta suluhisho la kudumu katika Jimbo la Mheshimiwa Hasunga. Sisi Serikali tunaendelea kuhakikisha kwamba jicho letu haliondoki pale kuhakikisha kwamba mradi huu unakamilika. 
Mheshimiwa Spika, mradi huu ulikuwa na changamoto mbili, tatu, lakini tunaelekea kuzikamilisha na zitakapokamilika, mtiririko wa fedha na kasi ya ufanyaji wa kazi itakuwa ni kubwa na hatimaye kazi hii itakamilika na wananchi wa eneo hilo watapata huduma ya maji safi na salama na yenye utoshelevu.   Ahsante sana. (Makofi)   
							
 
											Name
George Natany Malima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpwapwa
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Ichenjezya, Hasamba, Nwansana, Vwawa hadi Ilolo utakamilika na kuanza kutoa maji ya uhakika?
Supplementary Question 2
MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Mradi wa Maji wa Kisokwe – Idilo – Mazae ulioko katika Mji wa Mpwapwa?
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua uhitaji wa ukamilishaji wa miradi mingi inayoendelea na kuna miradi zaidi ya 1,000 chini ya Wizara ya Maji nchi nzima, miradi ya kimkakati, miradi ya kitaifa, mabwawa na kadhalika. Lengo letu ni kuhakikisha kwamba ndani ya mwaka huu wa fedha ifikapo Oktoba, basi miradi hii iwe imekamilika ikiwemo na miradi ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja. Ahsante sana. (Makofi)
 
											Name
Mashimba Mashauri Ndaki
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Magharibi
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Ichenjezya, Hasamba, Nwansana, Vwawa hadi Ilolo utakamilika na kuanza kutoa maji ya uhakika?
Supplementary Question 3
MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Spika, ni lini Serikali itawalipa wakandarasi wa Miradi ya Maji Kata ya Zanzuwi, Kata ya Mwamashimba na Kata ya Malampaka ambao wameomba kulipwa hela zao toka mwaka 2024 ili waendelee kukamilisha miradi ambayo iko kwenye maeneo hayo? (Makofi)
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Mashimba Ndaki kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mashimba Ndaki kwanza kwa ushirikiano anaotupatia Wizara ya Maji, lakini pili kwa kutoa ushirikiano tunapokuwa na miradi ndani ya jimbo lake na tatu ni kwa namna ambavyo anatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi. 
Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa kumekuwepo na madai ya wakandarasi katika Wilaya ya Maswa, lakini tumekuwa tukilipa hatua kwa hatua. Mpaka sasa madai ambayo wameshayaleta wakandarasi kutoka Maswa, tayari Katibu Mkuu ameshayapeleka Wizara ya Fedha, kwa ajili ya kupata idhini ya malipo ili waweze kuendelea na mradi huo na ukamilike kwa wakati.  Ahsante sana. (Makofi)    
							
 
											Name
Condester Michael Sichalwe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Momba
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Ichenjezya, Hasamba, Nwansana, Vwawa hadi Ilolo utakamilika na kuanza kutoa maji ya uhakika?
Supplementary Question 4
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kwa kunipatia nafasi. Mheshimiwa Naibu Waziri, tunakushukuru sana ulifanya ziara kwenye Jimbo la Momba tarehe 14 Januari, 2025. Ukaahidi miezi mitatu Mradi wa Msangano mpaka kufikia sasa tupate maji na Mradi wa Lwatwe, mwezi mmoja mpaka tupate maji, lakini mpaka sasa hivi hakuna ambacho kinaendelea. Ni nini kauli yako ya faraja kwa wananchi wa Jimbo la Momba?
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninatambua na ninafahamu kwamba nilikuwepo na Mheshimiwa Condester katika jimbo lake na tulifanya mkutano wa hadhara na Serikali ilitoa ahadi. 
Mheshimiwa Spika, ni kwamba, wakati tunatoa ahadi kulikuwa na miradi mingine iliyokuwa inaendelea ambayo pia ilikuwa inahitaji fedha kwa wakati huo huo. Pia, katika jimbo ambalo Serikali imepeleka miradi mingi ya maji katika kipindi cha miaka mitano ni pamoja na Jimbo la Mheshimiwa Condester. 
Mheshimiwa Spika, tunapokea changamoto hii na tutaendelea kuifanyia kazi ili kuhakikisha kwamba lazima ahadi ya Serikali kwa wananchi ni inatekelezwa. Sisi Wizara ya Maji tuko tayari kuhakikisha kwamba tunachukua hatua kali kwa viongozi wetu ambao tumewapa majukumu ya kutekeleza ili waweze kutekeleza kwa wakati na wananchi wapate huduma ya maji safi na salama.  Ahsante sana.  (Makofi) 
							
 
											Name
Suma Ikenda Fyandomo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Ichenjezya, Hasamba, Nwansana, Vwawa hadi Ilolo utakamilika na kuanza kutoa maji ya uhakika?
Supplementary Question 5
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Mradi wa Maji wa Kiwila ambao unategemewa sana na wananchi wa Mbeya Jiji pamoja na Mbalizi, mkataba wake ilikuwa uishe mwezi huu wa Aprili na Machiu. Sasa je, ni lini wananchi wa Mbeya Jiji watakamilishiwa mradi huo? Ukizingatia kauli kubwa ya Mama Samia Suluhu Hassan ni “kumtua ndoo mama kichwani.” Ninaomba majibu Wanambeya Jiji pamoja na Mbalizi wasikie. Ahsante. (Makofi)
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo:- 
Mheshimiwa Spika, ninatambua na Serikali inatambua umuhimu wa Mradi huu wa Kiwila. Ni mradi mkubwa, nimeshaenda kuutembelea na nimeuona. Pia, tunafahamu kabisa kwamba, wakati tunaanza kufanya kazi kulikuwa na baadhi ya changamoto kwenye source, kule kwenye intake, ambayo ndiyo iliyochelewesha. Pia, tunafahamu kabisa kwamba mradi huu ndiyo mwarobaini wa wana Mbeya na Jiji la Mbeya na Serikali tumejizatiti kuhakikisha kwamba mradi huu unakamilika kwa wakati ili Wananchi wa Jiji la Mbeya waweze kupata huduma ya maji safi na salama.  Ahsante sana.
SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, hapo kwenye wakati hapo, mmeshaongeza muda gani? Miezi sita, mwaka au miaka miwili? (Makofi)      
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ili Serikali itoe jibu la uhakika, ninaomba tulifanyie kazi halafu tutamrejea muuliza swali. Ahsante sana.  
							
 
											Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Ichenjezya, Hasamba, Nwansana, Vwawa hadi Ilolo utakamilika na kuanza kutoa maji ya uhakika?
Supplementary Question 6
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ni lini Serikali itakamilisha miradi inayojenga katika Bonde la Mwakaleli, hususan Kata za Luteba, Isange, Kandete na Mpombo? (Makofi)
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, miradi hiyo iko ndani ya muda wa mkataba na tunaamini kwamba mpaka kufikia kwa mujibu wa mkataba jinsi ambavyo umesainiwa, miradi hiyo itakuwa imekamilika. Ahsante sana.
 
											Name
Margaret Simwanza Sitta
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Urambo
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza:- Je, lini Mradi wa Maji wa Ichenjezya, Hasamba, Nwansana, Vwawa hadi Ilolo utakamilika na kuanza kutoa maji ya uhakika?
Supplementary Question 7
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niulize swali la nyongeza. Kutokana na shida kubwa ya maji tuliyonayo Urambo, je, ni lini maji kutoka Lake Victoria yatafika? (Makofi)
 
											Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
								NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali kama ifuatavyo:- 
Mheshimiwa Spika, ninatambua namna ambavyo Mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta anawapambania wana Urambo na tunatambua kwamba mradi huu ni extension ya Mradi wa Ziwa Victoria uliogharimu shilingi bilioni 680. Pia, tunatambua huu ni mradi wa extension ya kwenda Urambo, Sikonge pamoja na Kaliua. Ambapo una jumla ya package ya bilioni 143, lakini pia mradi huu umefikia ziadi ya 50% na sasa tunatarajia kwamba kabla mradi haujakamilika, tumetoa option ya kuhakikisha kwamba maeneo mengine yanaweza kuanza kupata huduma ya maji wakati mradi ukiwa unaendelea.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, namtoa hofu, tayari ma-engineer wetu wanafanyia kazi maelekezo haya na wananchi wataanza kupata maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria.  Ahsante sana.