Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Neema Kichiki Lugangira

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA K.n.y. MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa majibu ya tafiti zilizofanywa Kanda ya Ziwa kubaini visababishi vya kansa iliyokithiri?

Supplementary Question 1

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Spika, Pamoja na maelezo ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuzingatia kuwa katika Mikao ya Kanda ya Ziwa kuna shughuli nyingi za Sekta ya Madini na uchepushaji wa kemikali kwenda kwenye Ziwa Victoria unasemekana kuweza kuathiri samaki na dagaa ambazo jamii inayozunguka Ziwa Victoria wanakula. Hivyo, kuna uwezekano wa kuchangia katika ongezeko la kansa. Sasa je, Wizara ya Afya hamwoni ipo haja ya Serikali kuwa na chombo maalum cha kudhibiti masuala yote ya chakula, lishe na usalama wa chakula kwa maana ya food safety? Hilo ni swali la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa, Wizara ya Afya hapa kwenye majibu imeeleza kwamba inajikita katika kutoa elimu, ninaamini elimu hii ni pamoja na masuala ya usalama wa chakula kwa maana ya food safety. Je, Wizara haioni iko haja kwa Serikali kufuata miongozo ya dunia ikiwemo Shirika la Afya Duniani, kwamba masuala ya udhibiti wa usalama wa chakula kwa maana ya food safety yawe chini ya Wizara ya Afya na siyo chini ya TBS? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kuuliza masuala muhimu ya afya na muhimu sana kwa usalama wa afya zetu, lakini pia kwa usalama wa nchi yetu. Ninakushukuru sana Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Spika, kuhusu maswali yake mawili: swali la kwanza kama Serikali haioni sababu ya kuwa na chombo maalum cha kusimamia usalama wa chakula. Serikali ina chombo maalum ambacho kwa sasa masuala ya chakula yanasimamiwa na TBS. Pia, Serikali imekuwa inafanya kazi ya kina kuhakikisha uchafuzi unaofanyika na mambo hayo mengine ambayo yanaweza yakaleta madhara kwa binadamu yanasimamiwa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kuna usimamizi wa kina sana. Hata hivyo, ninakubaliana na wewe kwamba, bado kuna watu ambao sio wazuri na hawafuati zile sheria ambazo wenzetu wa afya, wenzetu wa mazingira na wenzetu wa maji wamezitoa katika kuchepusha vitu mbalimbali ambavyo vinaweza vikawa na madhara kwa binadamu. Kwa hiyo tutaendelea kuongeza nguvu katika kufuatilia eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, suala lake la pili, kwamba ni suala la kurudisha chakula kutoka TBS kuja TMDA kwa maana ya kuwa FDA kama ambavyo tulikuwa zamani. Kwanza, Mheshimiwa Mbunge isisahaulike kwamba suala hilo lilipitia hapa Bungeni na likaamuliwa na Bunge kwamba iende TBS. Sasa tunamwomba Mheshimiwa Mbunge aendelee kuipa Serikali muda ndani ya Wizara husika kuna mchakato unaoendelea wa kujadiliana kuona sababu ambazo zilisababisha ziende kule TBS kama inawezekana, basi tukatafuta sababu ya kuweza kurudisha kama ambavyo Bunge kwa wakati wote limekuwa likishauri. Tunaomba aendelee kutuvumilia mara nyingi tumesikia akilisimamia hilo, lakini kwa kweli mjadala unaendelea kwa ajili ya kutekeleza hilo. (Makofi)

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA K.n.y. MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa majibu ya tafiti zilizofanywa Kanda ya Ziwa kubaini visababishi vya kansa iliyokithiri?

Supplementary Question 2

MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa takwimu zinaonyesha idadi kubwa ya wagonjwa walioko Hospitali ya Ocean Road wakipata huduma kutokana na matatizo ya saratani wanatoka Kanda ya Ziwa na Hospitali ya Rufaa ya Bugando ina Kitengo cha Saratani. Ni kwa nini Serikali isiimarishe Kitengo hiki kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bugando ili kupunguza gharama kwa wagonjwa wa saratani wanaotumia gharama kubwa kwenda Hospitali ya Ocean Road? Ninashukuru. (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge. Utafiti unaonyesha baada ya hili swali kuwa linaibuka kila wakati na umefanyika utafiti unaonyesha wagonjwa wengi walioko Ocean Road wanatokea Kanda ya Kaskazini. Pamoja na hayo haizuii kwamba Serikali, imeshatoa zaidi ya shilingi bilioni nane kwenye Hospitali yetu ya Bugando kwa ajili ya kuboresha hili eneo la cancer. Kwa kweli lengo na maelekezo ya Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni sisi baada ya uboreshaji uliofanyika Ocean Road sasa tuanze kuboresha hospitali zote za kanda ikiwezekana kwamba wagonjwa wawe wanabaki kwenye hospitali zao za kanda, wachache sana wawe na sababu ya kuja Dar es Salaam, Ocean Road.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo swali la Mheshimiwa Mbunge ni zuri na linaenda kutekelezwa kwa nguvu sana na ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA K.n.y. MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa majibu ya tafiti zilizofanywa Kanda ya Ziwa kubaini visababishi vya kansa iliyokithiri?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa waathirika wa huu ugonjwa wa cancer, kuna wengi ambao hawana uwezo kwa gharama ya Bima ya Afya ...

SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati, uliza swali, nenda moja kwa moja.

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, Serikali inawasaidiaje wananchi ambao wanaugua cancer, hawana uwezo wa matibabu wala bima ya afya? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ndiyo maana wakati uliopita niliwahi kusema hapa kwa takwimu za miaka miwili iliyopita kwamba Serikali ilitumia shilingi bilioni 667 kwenye eneo la kusaidia watu wasioweza kulipia tiba. Pia, ni kweli kwamba, ni ukweli pamoja na kutumia shilingi bilioni 667 bado haijaweza kuwasaidia wote waliohitaji kupata hiyo huduma. Kwa hiyo, ndiyo maana tumekuja na Bima ya Afya kwa Wote, lakini tutaendelea kuongeza nguvu kwenye hilo na ndiyo maana tunasisitiza sana mapato ya ndani na Utalii Tiba. Tunaposisitiza Utalii Tiba ina maana watu wanaotoka nje kuja kutibiwa wanapoacha fedha ndani basi fedha hizo zinaenda kusaidia watu ambao hawajiwezi kama hao ambao Mheshimiwa Dkt. Kabati amesema.

Name

Tarimba Gulam Abbas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kinondoni

Primary Question

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA K.n.y. MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa majibu ya tafiti zilizofanywa Kanda ya Ziwa kubaini visababishi vya kansa iliyokithiri?

Supplementary Question 4

MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Spika, ninaomba nimuulize Mheshimiwa Naibu ...

SPIKA: Uliza tu swali, huna haja ya kuomba tena nimeshakupa nafasi.

MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Spika, ninataka kujua kuna taarifa kwamba mashine za PET Scans ziko pale Ocean Road. Swali, je, zimeshaanza kufanya kazi na ni wataalam wa aina gani ambao tuko nao kwa minajili ya mashine hizo?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli Mashine ya PET CT-Scan imeshafungwa na imeshaanza kazi. Kulikuwa tuna shida kidogo ya software fulani ambayo ilitakiwa ndani ya wiki mbili iwe imemalizwa ili huduma nyingine ziendelee, lakini imeshafungwa na imeanza kazi, lakini kuna software ambayo tunahitaji ifungwe pale ili uweze kufanya kwa capacity yake nzima. Imeanza kazi na ndiyo maana tumekuwa tukiwaambia mashine alizofunga Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, tuna uwezo hata wa ku-detect cancer inayokuja miaka mitano, miaka 10 ijayo.

Name

Felista Deogratius Njau

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA K.n.y. MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa majibu ya tafiti zilizofanywa Kanda ya Ziwa kubaini visababishi vya kansa iliyokithiri?

Supplementary Question 5

MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Spika, wagonjwa wengi wa saratani wanajulikana na ugonjwa huo wakiwa wameshafika stage za mbali kabisa na hivyo kuleta athari ya uhai wao. Nini mkakati wa Serikali kuhakikisha wanatoa elimu ili watu wengi waweze kupima mapema kabla ya kuathirika? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, miaka mitatu iliyopita kwa kweli swali la msingi alilosema dada yangu hapa lilikuwa hivyo, lakini baada ya Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kusambaza teknolojia na miundombinu mpaka kule chini, sasa kutoka 90% ya wagonjwa waliokuwa wanakuja ikiwa cancer imefika mbali sasa wameshapunguzwa kwa 78%. Maana yake mpaka mwaka unaofuata baadaye utaona wamepungua kabisa, kwa sababu sasa teknolojia iko chini na wataalam wameshushwa chini na uwezeshaji umeenda. Kwa hiyo hilo limeweza kushughulikiwa kwa kina kama ambavyo ungetamani. Kwa hiyo ripoti ndiyo hiyo.

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Primary Question

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA K.n.y. MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa majibu ya tafiti zilizofanywa Kanda ya Ziwa kubaini visababishi vya kansa iliyokithiri?

Supplementary Question 6

MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Spika, wagonjwa wa cancer wamekuwa wakiongezeka siku hadi siku. Je, Serikali haioni ni muda muafaka sasa kuona namna bora ya kuweza kutoa ruzuku kwa wagonjwa hawa waweze kuwa wanapata matibabu, kwa sababu wengi hawana uwezo wa kuweza kujitibia wenyewe? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, moja ya Sera yetu ni kuwatibu hawa wagonjwa bure, lakini suala sio kutoa ruzuku. Kama ambavyo nimeshasema kwenye swali la Mheshimiwa Dkt. Kabati, kuna utaratibu huo wa kuwasaidia, lakini inawezekana zamani watu walikuwa wanakufa kwa cancer, lakini hawajulikani. Hata hivyo, kwa sababu ya uboreshaji wa huduma za afya, sasa watu wanajulikana mapema na watu wamekuwa screened mapema na kujulikana tatizo ni nini. Pia, tutaendelea kukabiliana kuendelea kutoa elimu ili kupunguza sababu ya watu kupata cancer badala ya kuongeza ruzuku.

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Primary Question

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA K.n.y. MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza:- Je, lini Serikali itatoa majibu ya tafiti zilizofanywa Kanda ya Ziwa kubaini visababishi vya kansa iliyokithiri?

Supplementary Question 7

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, kwa nini Madaktari Bingwa ambao wangeweza kusaidia masuala ya cancer na wale wanaoenda kwa ajili ya zile huduma za kupeleka vijijini hawalipwi posho zao kupitia Bima ya Afya, kwamba hawatambuliki katika Bima ya Afya? Ahsante.

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nimelisikia hapa, sitegemei Bima ya Afya isiweze kuwalipa Madaktari ambao wanasaidia wagonjwa wa cancer. Mheshimiwa Ritta Kabati tutasaidiana anionyeshe specific ni nini kimetokea na ninataka kumhakikishia tutalitatua leo na kwisha na halitojirudia.