Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Shally Josepha Raymond
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. KHADIJA S. TAYA aliuliza:- Je, Serikali imeweka utaratibu gani wa kuwasaidia matibabu ya ngozi watu wenye Ualbino kutokana na Ugonjwa wa Saratani ya Ngozi kuongezeka?
Supplementary Question 1
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; ualbino unatokea kutokana na wazazi wa aina mbili kuwa zile chromosomes za aina fulani. Je, elimu inatolewa vipi ili hao watu wasiende tena kukutana au kuoana ili waongezeke kwa kasi? 
Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa vifaa hivyo umevitaja eneo linalofahamika zaidi ni Hospitali ya KCMC. Je, inawezekana kutoa vifaa hivyo kwenye Hospitali za Rufaa na kushusha kwenye vituo vya afya hadi kwenye dispensaries? (Makofi)
 
											Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
								NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo amekuwa akifanya kazi nzuri sana kwenye Wilaya zetu sisi Wabunge ambao tunatokea Mkoa wa Kilimanjaro, tunamshukuru sana dada yangu kwa jinsi ambavyo anawahudumia akinamama kwenye hili eneo lake. 
Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza, kwamba kuhamasisha watu ambao wana uwezekano wa kupata mtoto albino wasioane hilo ni gumu kidogo, kwa sababu wanaanza kupendana hata kabla ya kuanza kupima mambo mengine. Kwa hiyo sasa wakati mwingine na hili nalo ukilichukua kama Serikali, inabidi tuwe makini sana kwenye suala zima la unyanyapaa na mambo mengine yanayofanana na hayo. Tunalichukua kulitafakari, lakini ni ngumu sana, namna ya kulitekeleza japo sababu hizo zinajulikana.  Tunafikiri sio suala la kuzungumza sana ili kuondoa unyanyapaa na kupunguza mambo mengine ya aina hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, anasema KCMC. Kwanza nitumie fursa hii kuipongeza KCMC kwa sababu wao wamefika mbali wana kiwanda chao cha kuzalisha wenyewe hayo mafuta. Kwa hiyo, niwapongeze sana. Pia, niseme ndiyo maana tumeweka kwenye bidhaa zinazosambazwa na MSD, maana yake MSD inasambaza mpaka vituo vyetu vya afya, dispensary kuhakikisha tunapatikana. 
Mheshimiwa Spika, kikubwa ni kuwaomba ma-DMO pamoja na Wafamasia wa Wilaya katika hizi bidhaa inawezekana wakati mwingine hazifiki huko chini sio kwamba hazisambazwi. Mara nyingi wanachoangalia MSD ni maombi kutoka Wilaya husika. Niwahamasishe ma-DMO wawatambue watu wenye Ualbino kwenye maeneo yao halafu sasa waweze kuweka hizo bidhaa kwenye bidhaa wanazoagiza, ili waweze kupata huduma hukohuko kwenye wilaya zao.
							
 
											Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. KHADIJA S. TAYA aliuliza:- Je, Serikali imeweka utaratibu gani wa kuwasaidia matibabu ya ngozi watu wenye Ualbino kutokana na Ugonjwa wa Saratani ya Ngozi kuongezeka?
Supplementary Question 2
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, je, Serikali iko tayari kufanya mabadiliko ya mwongozo wa utoaji wa huduma za afya ili kuruhusu huduma za watu wenye ualbino na watu wenye ulemavu vifaa vyao viweze kupatikana kwenye ngazi ya wilaya na vituo vya afya? (Makofi)
 
											Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza hilo ni swali zuri sana na halihitaji kubadilisha Sheria, liko obvious kulingana na uwezo wa kituo husika. Kwa hiyo, ninachosema kwa Waganga wetu wa Mikoa na Waganga wetu wa Wilaya, ni kwamba watazame matatizo hayo ya watu wenye ualbino pamoja na wenye ulemavu kulingana na uwezo wa kituo ihakikishe kwamba vifaa husika vinapatikana kwenye eneo husika.
 
											Name
Halima James Mdee
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. KHADIJA S. TAYA aliuliza:- Je, Serikali imeweka utaratibu gani wa kuwasaidia matibabu ya ngozi watu wenye Ualbino kutokana na Ugonjwa wa Saratani ya Ngozi kuongezeka?
Supplementary Question 3
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, mashine ya PET Scan ni muhimu sana katika kutambua namna ambavyo cancer imesambaa mwilini na kuweza kujua ni namna gani inaweza kutibiwa. Sasa ninataka nijue, ninafahamu mashine ipo lakini changamoto iliyopo ni kuanza kufanya kazi, ninaomba tupate taarifa sahihi kuhusiana na hilo. (Makofi)
 
											Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Halima Mdee kwa namna ambavyo sio suala hili tu na masuala mengi ya afya na kijamii amekuwa akiyafuatilia kwa karibu. Hata hivyo, nimwambie PET Scan kweli ipo, lakini unazungumzia human resource ambao wataziendesha, kweli sasa hivi tunao, lakini hawatoshi. Sasa hivi tunavyozungumza kupitia Dkt. Samia Scholarship, kuna watu zaidi ya nane wako nje wanasoma kwa ajili ya kurudi kutoa huduma zinazofanana na hizo. Pia, software ambayo nayo ilikuwa ni tatizo imeshafanyiwa kazi tunategemea baada ya muda itakuwa imefungwa vizuri na huduma hiyo itatolewa kwa 100% ambayo ilikuwa inatolewa kwa 80% ya capacity ya mashine yenyewe.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved