Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:- Je, lini Serikali itatafsiri upya Liquor and Intoxication Act, 1968 ili kutoa fursa kwa Wakulima wa Korosho kupata kipato kwenye Gongo ya Mabibo?

Supplementary Question 1

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, kwanza nishukuru kwa majibu mazuri kabisa ya Serikali kuhusiana na suala hili, kwa sababu limekaa hapa mbele yetu na utakuwa shahidi kwa muda mrefu sana tukilijadili na malengo ni kwamba kuongeza ile value chain ili wakulima wa korosho waweze kujipatia mapato. Sasa Serikali ipo tayari kutoa elimu kwa wakulima wa korosho kutokana na hii sheria? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali ipo tayari. Kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, mara kadhaa tumemsikia Waziri akitoa hapa ufafanuzi, SIDO wana Idara ya Elimu kwa ajili ya kutumia teknolojia inayoweza kuongeza thamani katika mazao mbalimbali yanayozalishwa na wananchi wetu. Kwa hiyo, wakulima wa jimbo lako wanaweza wakatumia fursa hiyo ili kujiimarisha wakafanya kitu ambacho kinakubalika kwa mujibu wa Sheria. Ahsante.