Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza:- Je, lini TANAPA watatumia vizuri fursa za Misitu waliyonayo kunufaika na Biashara ya Carbon kama nchi nyingine zinavyonufaika?

Supplementary Question 1

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; je, ni lini Serikali itaanza utekelezaji wa mkakati madhubuti wa kutumia misitu iliyopo katika Mlima Meru Mkoani Arusha kwa ajili ya uwekezaji wa biashara hii?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; ni kwa namna gani mkakati huu wa Serikali utakwenda kunufaisha wananchi wa Mkoa wa Tanga katika Milima ya Usambara na Amani. Ninashukuru sana. (Makofi)

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, anaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kwa pamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, biashara hii ni biashara mpya ambayo inafanyika katika level ya Kimataifa, tunachofanya kama nchi kwa sasa ni kuhakikisha tunakuwa na umakini mkubwa katika kuweka sawa mambo yetu ndani ili mikataba hii tutakapoingia na makampuni haya ya Kimataifa isije ikawa ni tatizo kwetu kama nchi isipokuwa iweze kutunufaisha.

Mheshimiwa Spika, maeneo ya Mlima Meru ni eneo ambalo ni urithi wa Taifa, tusipokuwa makini katika mikataba yetu tunaweza kujikuta tumekabidhi haki ya kumiliki maeneo hayo kwa watu wachache na sisi mwisho wa siku tukashindwa kuyatumia kunufaika kwa njia nyingine. Kwa hiyo naomba Waheshimiwa Wabunge tuwe na subira wakati Serikali inachukulia jambo hili kwa umuhimu mkubwa ili mikataba hii isije kuwa janga iwe ni mikataba ya kuleta manufaa kwa Taifa letu.(Makofi)

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza:- Je, lini TANAPA watatumia vizuri fursa za Misitu waliyonayo kunufaika na Biashara ya Carbon kama nchi nyingine zinavyonufaika?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ninafikiri hii subira tunayoambiwa tuvute tunapoteza fursa ya kupata mapato kutokana na chanzo hiki. Kuna nchi nyingi tayari zinafanya biashara hii, kwa nini watu wetu wasiende kujifunza tukapata fedha Vijiji vyetu kule Moshi - Vunjo vimekosa cooperate social responsibility kutokana na biashara hii. (Makofi)

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, tuna utajiri wa maarifa katika nchi yetu na ndiyo maana tunasema subira yavuta kheri. Wataalam wetu wamekwisha kwenda kujifunza kwenye nchi nyingine tumeona makosa ambayo wenzetu wameyafanya na katika kujifunza huko ndiyo maana Tanzania imekuwa nchi ya kwanza katika Afrika kuwa na mwongozo thabiti wa kufanya biashara hii. Nimesema sasa hivi taasisi zetu zinaandaa mikataba itakayotuwezesha tusiingie kwenye matatizo.

Mheshimiwa Spika, naomba tuwe na subira ili tutoke vizuri kwenye jambo hili.

SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mheshimiwa Masauni.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuongezea majibu kwa maswali ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni sahihi kwamba kwenye biashara ya carbon kuna fursa pana sana ambayo inaweza ikasaidia nchi yetu kuweza kupata fedha, lakini kusaidia pamoja na jitihada za kidunia kupambana na mabadiliko ya tabianchi, lakini kuna hatua kadhaa ambayo Serikali zimechukua katika kufanikisha hilo hasa tukitilia maanani...

Mheshimiwa Spika, nasema ni sahihi kwamba kwenye biashara ya carbon kuna fursa kubwa sana inayoweza kusaidia nchi yetu kupata fedha, lakini kupambana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi. Ni sahihi kwamba bado kama Taifa hatujatumia vya kutosha fursa hiyo, kwa hiyo katika kuchukua hatua Serikali imefanya yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza, Bunge lililopita kama utakumbuka wakati tumepitisha mabadiliko ya Sheria ya Mazingira, kwa mara ya kwanza tuliweza kukitambua Kituo cha Kuratibu Biashara ya Carbon kilichopo Morogoro kisheria, lakini sasa tupo katika hatua za kukiimarisha kituo hicho kwa maana ya kuweza kuunda board na management ili kiweze kufanya majukumu yake vizuri.

Mheshimiwa Spika, hali kadhalika, hizi siku chache zilizopita tuliunda Kamati ya wataalam ya kushauri namna bora ya kuweza kufaidika na biashara hii lengo ni kuhakikisha kwamba uwekezaji katika maeneo yote muhimu ikiwemo miradi mikubwa ya kimkakati na maeneo ambayo bado yana fursa ya kuweza kufanyika biashara hii tunaweza kuitumia vizuri.

Mheshimiwa Spika, ninaungana na Mheshimiwa Naibu Waziri kuwaomba Waheshimiwa Wabunge wawe na subira wakati Serikali inajipanga vizuri kuhakikisha kwamba katika muda mchache unaokuja tuweze kunufaika na biashara hii katika maeneo yote yenye fursa katika eneo hili. Ninakushukuru. (Makofi)

Name

Priscus Jacob Tarimo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Mjini

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza:- Je, lini TANAPA watatumia vizuri fursa za Misitu waliyonayo kunufaika na Biashara ya Carbon kama nchi nyingine zinavyonufaika?

Supplementary Question 3

MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Swali la kwanza; kwa sababu Serikali ipo kwenye utaratibu wa kukamilisha hiyo sheria na miongozo; je, wapo tayari sasa kuhakikisha kwamba hayo manufaa yatakayopatikana yatashirikisha Halmashauri ambazo zimezunguka misitu hiyo kwa mfano Msitu wa Rau pale Moshi upo ndani ya Moshi ndiyo wanaoulinda, wapo tayari sasa kwamba hayo manufaa yatumike na Halmashauri pia. (Makofi)

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, Serikali ipo tayari. (Makofi)

Name

Rehema Juma Migilla

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ulyankulu

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza:- Je, lini TANAPA watatumia vizuri fursa za Misitu waliyonayo kunufaika na Biashara ya Carbon kama nchi nyingine zinavyonufaika?

Supplementary Question 4

MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Serikali kusema kwamba wanasubiri mikataba tayari Wilaya ya Tanganyika wameshaanza kufanya biashara hii ya hewaukaa na sisi kama Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua tumekwenda hivi juzi kujifunza kuhusu uvunaji wa hewaukaa. Je, hawa Wilaya ya Tanganyika wanatumia mikataba gani ambayo haiwezekani kutumika kwenye Wilaya zingine? (Makofi)

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali ya nyongeza ya Waheshimiwa Wabunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nilizungumza kwamba sheria ipo tayari, Bunge lililopita sheria imepitishwa, lakini hali kadhalika kanuni ilikuwepo kabla hata sheria haijatungwa ambayo imeeleza namna ambavyo Halmashauri zetu zinapata faida kiasi gani na Serikali inapata kiasi gani, ndiyo maana kama alivyozungumza Mheshimiwa Mbunge kule Wilaya ya Tanganyika wanapata mgao kulingana na kanuni hiyo iliyopo sasa hivi.

Mheshimiwa Spika, changamoto kubwa iliyopo ni kwamba kama Serikali haturidhiki juu ya utaratibu mzima juu ya uendeshaji wa biashara hii, tunadhani kwamba katika biashara hii inaweza ikaendeshwa vizuri zaidi na Serikali ikapata tija zaidi. Vilevile tunaamini kwamba kuna fursa nyingine pana zaidi katika hii nchi haijatumika ipasavyo. Kwa hiyo mikakati ambayo tumechukua au hatua tulizochukua zinalenga katika kutatua changamoto ya masuala mengine ili kwa ujumla wake Serikali iweze kunufaika vizuri ziadi katika biashara hii. (Makofi)