Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question

MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka gari la Zimamoto Wilaya ya Nyang’hwale?

Supplementary Question 1

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kuipongeza Serikali kwa kutupatia gari la Zimamoto Wilaya ya Nyang’hwale, lakini pia niwapongeze Jeshi la Zimamoto Wilaya ya Nyang’hwale wanafanya kazi kwa kujituma pamoja na kwamba wapo wachache naomba niwatambue tu wa kwanza kiongozi wa Sajini Abdalah Mwinyimvua, Konstabo Fadhili Kipilipili, Konstabo Bichi Philemoni wanafanya kazi kubwa sana kipindi hasa cha masika yanapotokea mafuriko.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; je, Serikali ipo tayari kutupatia gari kwa ajili ya Maafisa hawa waweze kufanya kazi ya kuzunguka na kutoa elimu kwenye taasisi mbalimbali?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, Serikali ipo tayari kusambaza au kutengeneza miundombinu kwa ajili ya maji ya dharura ya zimamoto katika Makao Makuu ya Wilaya ya Nyang’hwale?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Mbunge kwa pongezi alizotoa kwa Askari ambao wanafanya kazi nzuri sana katika Wilaya ya Nyang’hwale.

Mheshimiwa Spika, kuhusu maswali mawili ya nyongeza, swali la kwanza, kwa sasa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesambaza magari katika mikoa yote nchini, hatua inayofuata ni kusambaza magari kwenye wilaya zote ikiwepo Wilaya ya Nyang’hwale.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, tayari Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeshafanya vikao vitatu na mamlaka za maji ili kuhakikisha kwamba wilaya zote za Mkoa wa Geita zinapata fire hydrants ikiwepo Wilaya ya Nyang’hwale.

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka gari la Zimamoto Wilaya ya Nyang’hwale?

Supplementary Question 2

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Ngara hatuna gari la zimamoto ningependa kujua ni lini Serikali itatupatia gari la zimamoto na hili swali nimeuliza mara ya tatu katika Bunge lako Tukufu? Ahsante sana. (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Oliver, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu na msingi tayari Serikali imeshaagiza magari 150 kwa ajili ya kupatia Zimamoto Wilaya zote nchini, ikiwemo Wilaya ya Ngara. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Robert Chacha Maboto

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda Mjini

Primary Question

MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka gari la Zimamoto Wilaya ya Nyang’hwale?

Supplementary Question 3

MHE. ROBERT C. MABOTO: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali italeta gari ya zimamoto katika Halmashauri ya Mji wa Bunda? Ninakushukuru.

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Robert Maboto, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali tayari imeshaagiza haya magari 150 kwa ajili ya Wilaya zote ikiwepo Wilaya ya Bunda pia. Ahsante sana.