Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE K.n.y. MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza kununua mahindi ya wananchi wa Jimbo la Ngara kupitia NFRA?

Supplementary Question 1

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ni lini Serikali itawatafutia soko la uhakika wakulima wa vanila, Wilayani Kyerwa?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, natambua jitihada kubwa inayofanywa na Mbunge kuhusu zao la vanila siku zote na moja ya jukumu kubwa ambalo sisi, kama Wizara, tunalo sasahivi ni kuhakikisdha kwamba, tunapata soko la uhakika kwa kutumia wadau mbalimbali. Kwa hiyo, tumeshaagiza na tumepeleka maelekezo katika balozi zote nje ya nchi kutafuta wadau kuja kuwekeza hapa nchini, kwa ajili ya zao la vanila. Ahsante sana.

Name

Mwantumu Mzamili Zodo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE K.n.y. MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza kununua mahindi ya wananchi wa Jimbo la Ngara kupitia NFRA?

Supplementary Question 2

MHE. MWANTUMU M. ZODO: Mheshimiwa Spika, je, ni lini NFRA watakwenda kununua mahindi Handeni, ambao wamekuwa wakitoa ahadi kila mwaka kwa wananchi na hawaendi? Ahsante sana.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kwamba, NFRA tayari wameshafanya tathmini katika maeneo yote ambayo tunapaswa kununua mahindi likiwemo eneo la Handeni. Kwa hiyo, katika mwaka huu wa fedha unaokuja tutatimiza kwa sababu, sasa hivi lengo letu kubwa ni kununua tani milioni moja za mahindi peke yake. Ahsante sana.

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE K.n.y. MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza kununua mahindi ya wananchi wa Jimbo la Ngara kupitia NFRA?

Supplementary Question 3

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali ama NFRA itaanza kununua sukari, ili kuwaepusha wakulima na bei ndogo ya kiwanda cha sukari inayolipa kwa wakulima wa muwa sasa hivi kwa kisingizio cha kwamba, sukari inabaki na hakuna soko? Ahsante.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, moja; mwaka jana Serikali kupitia Bunge lako Tukufu tulifanya mabadiliko ya Sheria ya Bodi ya Sukari kuruhusu NFRA kununua sukari na kuhifadhi, kwa ajili ya wakati wa dharura. Kwa hiyo, tumeshatimiza na tumeshaandaa kanuni, maana yake ni kuanzia sasa tutaanza kununua zinazotokana na viwanda vinavyozalisha sukari hapa nchini, hususan, katika Jimbo lako la Kilombero. Ahsante sana.

Name

Eric James Shigongo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buchosa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE K.n.y. MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza kununua mahindi ya wananchi wa Jimbo la Ngara kupitia NFRA?

Supplementary Question 4

MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kuniona. Wakati wa ziara ya Mheshimiwa Rais katika Jimbo la Sengerema nilizungumza na Mheshimiwa Naibu Waziri kuhusu kununua mahindi Buchosa na akampigia Mkurugenzi wa NFRA, Mr. Komba, wakasema wataanza kununua, lakini mpaka sasa hawajaanza kununua. Ningetaka kufahamu sasa, ni lini wataanza kununua mahindi Buchosa? Ahsante sana.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kwamba, kama nilivyoeleza hapo awali, mwaka huu NFRA wamefanya tathmini katika mikoa yote 26 na maeneo yote nchini ambayo tunapaswa kuweka vituo, kwa ajili ya kununua mahindi likiwemo Eneo la Buchosa analotokea Mheshimiwa Mbunge. Kwa hiyo, mwaka huu kutakuwa na utekelezaji halisia. Ahsante sana.