Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Omari Mohamed Kigua
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilindi
Primary Question
MHE. OMARI M. KIGUA K.n.y MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuhamasisha watumiaji wa Tanzania kununua bidhaa na huduma zinazozalishwa hapa nchini?
Supplementary Question 1
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na ninashukuru kwa majibu mazuri tu ambayo Serikali imetoa juu ya eneo hili. Ni ukweli usiyopingika kwamba kuhamasisha utumiaji bidhaa za ndani kwa kiasi kikubwa utaenda kupunguza matumizi ya foreign currency kwa maana fedha za kigeni, lakini hakuna jitihada kubwa zimefanyika kwa upande wa Serikali kuhakikisha kwamba bidhaa hizi za ndani wanapewa elimu ya kutosha ili ziwe na quality au thamani ya hali ya juu.
Mheshimiwa Spika, nini mpango mkakati sasa wa Serikali kuhakikisha kwamba bidhaa za ndani utayarishaji wake na packing inakuwa ni nzuri ili wananchi waweze kununua kwa kiasi kikubwa sana?  Ahsante. (Makofi)
 
											Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
								NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Kigua kwa kazi kubwa anayoifanya kwa Sekta hii ya Biashara na umekuwa ukifuatilia mara nyingi sana kuona tunaendelea kuboresha biadhaa zetu ziwe na ubora, lakini pia ziwe shindani.
Mheshimiwa Spika, nikuhakikishie wewe pamoja na Bunge lako Tukufu kwamba Serikali tayari ina mipango mahsusi, moja ni kupitia maonesho yetu ambayo hasa ndiyo yanahamasisha ubora wa bidhaa zetu kwa sababu zinapoenda kwenye maonyesho yale kupitia kama ile niavyosema Sabasaba na TIMEXPO maana yake bidhaa zetu zinashindana na bidhaa za nje, tumeshaona tayari wananchi wananunua wapenda bidhaa zetu.
Mheshimiwa Spika, Serikali tayari imetenga fedha mahsusi kupitia Shirika letu la Kuendeleza Viwanda Vidogo Vidogo Nchini - SIDO pia kwa kushirikiana na TBS kwa maana ya Shirika la Viwango Tanzania ili kuwasaidia wazalishaji wa ndani wapate teknolojia nzuri lakini kuwawezesha ili wawe shindani kwa kuwawekea nembo ya ubora ili bidhaa zao ziweze kuwa shindani katika masoko ya ndani, lakini pia na masoko ya nje. 
Mheshimiwa Spika, zaidi tayari tuna Biashara App ambayo yenyewe inasaidia kutangaza bidhaa zinazozalishwa ndani kwa Watanzania ili waweze kuona na kujua bidhaa moja inapatikana wapi kwa bei gani, lakini na ubora kama ulivyosema kwenye bidhaa hizo.  Ninakushukuru sana.
							
 
											Name
Janeth Elias Mahawanga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. OMARI M. KIGUA K.n.y MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuhamasisha watumiaji wa Tanzania kununua bidhaa na huduma zinazozalishwa hapa nchini?
Supplementary Question 2
MHE. JANETH E. MAHAWANGA: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti uingizwaji wa bidhaa kutoka nje ambao unaathiri ushindani wa wazalishaji wa bidhaa za ndani? (Makofi)
 
											Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
								NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Nimpongeze sana dada yangu Mheshimiwa Janeth Mahawanga kwa swali zuri. Moja ya maeneo ambayo Serikali imeweka msisitizo na mkazo mkubwa ni kudhibiti bidhaa ambazo hazina ubora kutoka nje. Tayari tuna taasisi zetu ikiwemo hii taasisi ya kuhamasisha ushindani (FCC - Fair Competition Comission) Tume ya Ushindani ambayo yenyewe inaratibu na kuhakikisha bidhaa zinazotoka nje zinaingia zikiwa katika ubora unaotakiwa.
 Mheshimiwa Spika, pili, kupitia Shirika letu la Viwango Tanzania - TBS nao pia tunathibiti kuhakiki ubora wa bidhaa zinazotoka nje ili kulinda bidhaa zetu za ndani. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inahakikisha tunafuatilia hasa mipakani na hasa hii mipaka ambayo ni vipenyo ambavyo si rasmi vinavyotumika kuingiza bidhaa hizi ambazo hazina ubora.
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved