Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Venant Daud Protas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Igalula
Primary Question
MHE. VENANT D. PROTAS K.n.y. MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: - Je, lini TARURA itaweza kutengeneza barabara zenye viwango zisizoharibika kipindi cha mvua?
Supplementary Question 1
MHE. VENANT D. PROTAS: Mheshimiwa Spika, ahsante, mwaka 2023/2024 kutokana na mvua nyingi kunyesha barabara nyingi zilipata hitilafu ikiwemo Barabara ya Goweko – Ndebelwa – Tabora Mjini, Barabara ya Izumba – Mpumbuli na Barabara ya Loya – Mabeshi. Pamoja na udharura wake, tulileta kwa hati ya dharura mpaka leo barabara hizi hazijatengenezwa.
Je, nini mkakati wa Serikali kuweka mikakati madhubuti ili pindi barabara hizi zinapoharibika zinaweza kupitika muda wote ili wananchi wasipate adha kama wanavyopata adha mpaka waakti huu?
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa kuwa Mheshimiwa Waziri amekiri kuwa barabara ni za udongo na mvua nyingi zikinyesha zinapata hitilafu; je, Wizara hawaoni kama katika fedha mnazoleta za TARURA kila halmashauri, basi tuwe tunakata 10% ambayo tunaweka kwenye mfuko maalum ili ikitokea dharura, zile fedha ziwepo ili zikatatue kutokana na udharura wake? 
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali yote mawili ya Mheshimiwa Mbunge kwa pamoja kwamba kwanza, Serikali inaweka kipaumbele kikubwa sana katika kuhakikisha kuwa inaimarisha miundombinu ya barabara hizi za wilaya zinazosimamiwa na TARURA. Ni dhahiri kwamba mvua nyingi zinazojitokeza kutokana na mabadiliko ya tabianchi zimesababisha barabara zetu ziweze kuharibika na kuleta adha kwa wananchi. 
Mheshimiwa Spika, Serikali inachukua jitihada za makusudi kabisa ili kuhakikisha kwamba inachukua hatua za dharura pindi pale mawasiliano yanapokuwa yamekatika kwenye barabara zetu. Mathalani, Mheshimiwa Mbunge ametaja katika jimbo lake barabara hizi ambazo zimeathirika katika mwaka wa bajeti 2023/2024 ninaomba kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inaendelea kuhakikisha kwamba inazifikia hizi barabara na kuhakikisha kwamba inachukua hatua za dharura kuzikarabati na kuzijenga na kuleta kuunganisha mawasiliano ambayo yamekatika ili wananchi wetu wasiweze kupata adha.
Mheshimiwa Spika, pia Serikali inatenga bajeti maalum kabisa ya dharura kila mwaka wa bajeti. Mathalani, katika mwaka 2023/2024 Serikali ilitumia zaidi ya shilingi 131,000,000,000 kama fedha ya dharura kwa ajili ya kuhakikisha kuwa inarudisha mawasiliano katika maeneo ambayo mawasiliano yamekatika. 
Mheshimiwa Spika, katika mwaka huu wa bajeti, Bunge hili lilipitisha nyongeza ya bajeti ya dharura ya TARURA shilingi 50,000,000,000; na mpaka sasa katika mwaka wa fedha huu tuliokuwa nao, tuna shilingi 71,000,000,000 ambazo zimetumika kwa ajili ya kuchukua hatua za dharura za kurudisha mawasiliano katika maeneo ambayo mawasiliano yamekatika. 
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuchukua hatua zote za msingi kuhakikisha inaendelea kuimarisha miundombinu ya barabara hizi muhimu kabisa ambazo zinawasaidia wananchi katika shughuli zao za kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuchukua hatua zote za msingi kuhakikisha inaendelea kuimarisha miundombinu ya barabara hizi muhimu kabisa ambazo zinawasaidia wananchi katika shughuli zao za kiuchumi na ambazo zinawawezesha kufikia huduma za msingi kabisa za kijamii.
							
 
											Name
Sophia Hebron Mwakagenda
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. VENANT D. PROTAS K.n.y. MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: - Je, lini TARURA itaweza kutengeneza barabara zenye viwango zisizoharibika kipindi cha mvua?
Supplementary Question 2
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya swali la nyongeza. 
Kwa kuwa Wilaya ya Rungwe ni wilaya yenye mvua nyingi, Serikali italeta lini fedha za ziada kwa ajili ya kutengeneza barabara zinazoharibika mara kwa mara?
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita imekuwa ikifanya uwekezaji mkubwa sana kwenye kuimarisha barabara zetu hizi za wilaya zinazosimamiwa na TARURA. Utaona katika mwaka wa fedha 2020/2021 bajeti ya TARURA ilikuwa ni shilingi bilioni 275 lakini wakati huu tunavyozungumza tunatarajia katika mwaka wa fedha 2025/2026 bajeti ya TARURA itakuwa ni shilingi trilioni 1.18. Kwa hiyo, unaona kabisa dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita kuendelea kuwekeza katika kuimarisha barabara hizi za muhimu.
Mheshimiwa Spika, ongezeko hili la bajeti linaonekana katika wilaya. Kila wilaya imepata nyongeza ya bajeti ya TARURA kwa ajili ya kuhudumia miundombinu ya barabara hizi za msingi kabisa za TARURA. Kwa hiyo, ninaomba nikuhakikishie Mheshimiwa Sophia Mwakagenda hata katika Wilaya ya Rungwe na yenyewe inanufaika na ongezeko la bajeti ambalo linalenga kwenda kuimarisha barabara hizi. Serikali itaendelea na jitihada hizi ili kuhakikisha wananchi wanapata barabara bora zaidi ambazo zinawawezesha kufanya shughuli zao za kiuchumi, lakini kufikia huduma za msingi za kijamii. (Makofi)
							
 
											Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. VENANT D. PROTAS K.n.y. MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: - Je, lini TARURA itaweza kutengeneza barabara zenye viwango zisizoharibika kipindi cha mvua?
Supplementary Question 3
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, ahsante, Jimbo la Tarime Vijijini lina mvua nyingi, udongo ni tifutifu. Ni kwa nini Serikali isitoe maelekezo mahususi kwa bajeti hiyo hiyo iliyopo, lakini kule waweke changarawe wasiweke udongo hata kama ni kilometa moja, meta 500 ili mvua ikinyesha watu wasikwame kufanya shughuli za kiuchumi?
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Serikali inahakikisha kwamba kila mwaka wa bajeti fedha zinapelekwa kwa ajili ya kuhudumia miundombinu ya barabara hizi muhimu kabisa za wilaya zinazosimamiwa na TARURA. Malengo ambayo yamewekwa na TARURA ni kuhakikisha kila mwaka kila wilaya inajengewa angalau kilometa moja ya lami, lakini pia kuna matabaka mengine ya barabara zetu hizi kwa maana ya changarawe na udongo. 
Mheshimiwa Spika, Serikali ina lengo la kuhakikisha kwamba inaendelea kuongeza mtandao wa barabara za lami ambazo kimsingi zinaishi muda mrefu zaidi kuliko matabaka haya mengine. Vilevile Serikali itaendelea kuhakikisha inapeleka fedha za kutosha kwa ajili ya kuhakikisha tabaka la lami linaongezeka, lakini tabaka la changarawe linaongezeka zaidi kuliko tabaka la udongo kwa maana matabaka haya mawili yanaishi muda mrefu zaidi kuliko tabaka la udongo. 
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaomba nikuhakikishie Mheshimiwa Mwita Waitara hata Tarime Vijijini lengo la Serikali ni kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara hizi za wilaya na hasa kwa matabaka ambayo yanaishi muda mrefu zaidi, Serikali italeta fedha kuhakikisha inaendelea kuimarisha miundombinu.
							
 
											Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. VENANT D. PROTAS K.n.y. MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: - Je, lini TARURA itaweza kutengeneza barabara zenye viwango zisizoharibika kipindi cha mvua?
Supplementary Question 4
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa kuwa barabara nyingi za TARURA katika Wilaya ya Kilolo zimekuwa hazipitiki kabisa wakati wa mvua. Je, ni kwa nini Serikali isifanyie upembuzi yakinifu wa yale maeneo machache tu ambayo hayapitiki wakati wote ili zijengwe kwa kiwango cha zege?
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
								NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikihakikisha inajenga miundombinu imara zaidi katika barabara zetu hizi za TARURA na lengo ni kuhakikisha kwamba barabara zinaishi muda mrefu zaidi, lakini zinapitika katika kipindi cha mwaka mzima. Serikali imekuwa ikifanya tathmini na kubaini maeneo ambayo ni korofi na kuweza kuyajengea miundombinu ambayo inaweza kustahimili mazingira ya mvua. 
Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati kwamba huo ndio mpango wa Serikali, kwenye maeneo ambayo ni korofi Serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara kwa tabaka la lami na maeneo mengine tabaka la zege na Serikali itaendelea kufanya hivyo hata katika Jimbo la Kilolo.
							
 
											Name
Kenneth Ernest Nollo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bahi
Primary Question
MHE. VENANT D. PROTAS K.n.y. MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: - Je, lini TARURA itaweza kutengeneza barabara zenye viwango zisizoharibika kipindi cha mvua?
Supplementary Question 5
MHE. KENNETH E. NOLLO: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru, junction ya Mayamaya - Mkondai paliharibika box culvert na kuvunja mawasiliano kati ya vijiji hivyo viwili, lakini Serikali tayari imeshapata mkandarasi na mkandarasi yule hajaripoti site. 
Je, ni lini Serikali inaweza ikafanya aende haraka ili kuondoa huu mkanganyiko ambapo sasa hakuna mawasiliano ya kwenda kijiji kinachofuata?
 
											Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kumwagiza Meneja wa TARURA wa Mkoa wa Dodoma akishirikiana na Meneja wa TARURA wa Wilaya ya Bahi kuhakikisha kwamba mkandarasi huyu ambaye amepewa kazi ya ujenzi wa kazi hii ya dharura aweze kuripoti site na aweze kuanza utekelezaji wa ujenzi wa barabara hii au matengenezo ya barabara hii haraka iwezekanavyo kwa mujibu wa mkataba.