Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuunganisha barabara kutoka Nyamilangano – Ushetu hadi Kaliua Tabora?
Supplementary Question 1
MH. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa usanifu wa kina utakamilika baada ya miezi 12; je, upatikanaji wa fedha na kuanza ujenzi utachukua miezi mingapi? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; barabara ya kutoka Kolandoto – Mhunze kwenda Mwangongo imekuwa ni kero kwa wananchi na majibu yamekuwa ni usanifu wa kina kila wakati. Je, ni lini Serikali itaanza kujenga hii barabara?
 
											Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
								NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilisha usanifu ndipo tunapoweza kujua gharama ya barabara na tukishakamilisha maana yake ni kwamba tutaiweka kwenye mpango wa kuijenga hii barabara baada ya kuwa tumekamilisha usanifu. Kwa hiyo, tuna uhakika tunapofanya usanifu maana yake kinachofuata ni kutafuta fedha kuanza kuijenga hiyo barabara.
Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Kolandoto – Mwangongo swali hili limejitokeza mara kadhaa na tumeshasema tumekamilisha usanifu na katika mpango wa bajeti wa mwaka huu barabara hiyo imepangiwa fedha kwa ajili ya maandalizi ya kuanza kuijenga kwa kiwango cha lami, ahsante. 
							
 
											Name
Yahaya Omary Massare
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Magharibi
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kuunganisha barabara kutoka Nyamilangano – Ushetu hadi Kaliua Tabora?
Supplementary Question 2
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, Barabara ya Mlongoji kwenda Lulanga, mkandarasi anayejenga amesimama kwa muda mrefu inapata mwaka sasa ambayo inaunganisha Mkoa wa Singida na Tabora.
Je, ni lini Serikali itampa pesa mkandarasi huyu ili arudi barabarani na iweze kupitika vizuri? Maana yake sehemu wanayopita wananchi sasa ni mbaya kuliko kiasi. (Makofi)
 
											Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
								NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwanza nimwelekeze Meneja wa Mkoa wa Singida kuhakikisha kwamba barabara hiyo inapitika kwa sababu ni wajibu wa mkandarasi aliyepo site kuhakikisha barabara ambayo anaijenga inapitika, lakini kuhusu upatikanaji wa fedha nimhakikishie Mbunge tulishapokea hati za madai na tulishaziwakilisha Hazina kwa ajili ya kumlipa huyo mkandarasi ili aweze kuendelea na kazi, ina maana tutakapopata hiyo fedha tutamlipa ili aweze kurejea site na kuanza kazi. Ahsante. (Makofi)
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved