Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Josephat Sinkamba Kandege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kalambo

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami barabara kutoka Mji Mdogo wa Laela – Mwimbi hadi Matai kuunganisha na Barabara ya Kasanga?

Supplementary Question 1

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya kututia matumaini ya Serikali naomba nielewe; je, kuna uwezekano wa kufupisha muda ili badala ya kutumika mwaka mzima katika kufanya hicho ambacho kinasemwa na Serikali ikatumika muda mfupi zaidi?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Mheshimiwa Naibu Waziri anaijua vizuri barabara ya kutoka Matai kwenda Kasesha boarder Zambia mpaka sasa hivi mkandarasi hayupo kwa sababu hajalipwa fedha. Je, Serikali ipo tayari kuhakikisha kwamba inamlipa fedha ili arudi kumalizia kazi ile? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kandege, Mbunge wa Kalambo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, wakati wa kufanya usanifu vigezo vyote vimekuwa vimeangaliwa kwamba barabara hii itachukua muda gani. Kwa hiyo, kwa wataalam walivyokadiria itachukua mwaka mmoja labda kutokee mazingira mengine inaweza ikaongezeka ama ikapungua kulingana na mazingira, lakini kwa upande wa watalam ni mwaka mmoja kwa maana ya miezi 12.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Matai – Kasesha tulisema katika bajeti lakini pia Wizara ya Fedha imesema kwamba miradi yote ambayo ilikuwa imesimama fedha itaanza kulipwa ili kazi ziendelee ikiwa ni pamoja na barabara hii ya Matai – Kasesha. Ahsante. (Makofi)

Name

Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami barabara kutoka Mji Mdogo wa Laela – Mwimbi hadi Matai kuunganisha na Barabara ya Kasanga?

Supplementary Question 2

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona; ni lini Serikali itajenga Barabara ya Kigonsera – Matili – Mbaha yenye urefu wa kilometa 56 ni barabara ambayo inakwenda nyumba kwa Makamu wa Rais ajaye Mheshimiwa Dkt. Emmanuel John Nchimbi? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, moja ni kwamba usanifu tumeshafanya wa barabara hii, lakini pia barabara hii inapita kwenye miinuko, maeneo mengi korofi tumeshayajenga kwa kiwango cha zege, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tunatafuta fedha ili hiyo barabara iweze kujengwa yote kwa kiwango cha lami. Ahsante. (Makofi)

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami barabara kutoka Mji Mdogo wa Laela – Mwimbi hadi Matai kuunganisha na Barabara ya Kasanga?

Supplementary Question 3

MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, Barabara ya Lyazumbi – Kabwe – Poti – Namanyeni – Kipili - Poti lini zitaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante na nimshukuru Mheshimiwa Aida Khenani amekuwa anaulizia barabara hii. Hii barabara tumeshaifanyia usanifu na inaenda kwenye Bandari ya Kabwe, lakini tulichofanya tumekuwa tunasema wakati tunatafuta fedha kuijenga yote ilikuwa kwanza kuimarisha makalavati na madaraja ili yaweze kupitisha magari makubwa yanayokwenda bandarini wakati Serikali inatafuta fedha.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Serikali inatafuta fedha ili tuweze kuijenga hiyo barabara yote kwa kiwango cha lami kwa sababu tumeshawekeza kwenye Bandari ya Kabwe ili iweze kufanya kazi, ahsante. (Makofi)

Name

Stanslaus Shing'oma Mabula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyamagana

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami barabara kutoka Mji Mdogo wa Laela – Mwimbi hadi Matai kuunganisha na Barabara ya Kasanga?

Supplementary Question 4

MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Spika, ahsante na napenda kumuuliza Mheshimiwa Waziri, barabara ya kutoka Mwanza Mjini kuelekea Usagara kupitia Kata za Buhongwa – Butimba – Mkuyuni – Igogo inaendelea kuwa finyu sana na tunazo taarifa kwamba mkandarasi alishapatikana. Kutokana na Daraja la JPM kukamilika traffic imekuwa kubwa sana na barabara hii inaingiza magari zaidi ya 15,000 kwa siku.

Sasa Serikali haioni umuhimu wa haraka kuhakikisha kwamba mkandarasi anatangazwa ili aanze kazi mara moja? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mabula, Mbunge wa Nyamagana kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tunatambua ni kweli Mji wa Mwanza umepanuka na magari yameongezeka na ndiyo maana Serikali ilishapanga kujenga njia nne kutoka Mwanza – Igogo – Nyegezi – Buhongwa hadi Usagara kwa njia nne na tunavyoongea sasa hivi tuko kwenye majadiliano na mkandarasi ambaye ataijenga hiyo barabara. Kwa hiyo, tunafahamu na hiyo barabara ipo kwenye mpango kuanza kuijenga mara moja na ndiyo maana mkandarasi ameshapatikana tuko kwenye majadiliano naye. Ahsante.

Name

Shamsia Aziz Mtamba

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Mtwara Vijijini

Primary Question

MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami barabara kutoka Mji Mdogo wa Laela – Mwimbi hadi Matai kuunganisha na Barabara ya Kasanga?

Supplementary Question 5

MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Spika, barabara ambayo inakwenda kwenye visima vya gesi barabara ya uchumi na barabara ya ulinzi lini zitajengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, barabara aliyoitaja ni muhimu kiuchumi na tumeshaipangia fedha kwa ajili ya kufanya maandalizi ya kuijenga, lakini kwa maana ya usanifu nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tumeshaikamilisha tunatafuta fedha tuanze kuijenga sasa yote kwa kiwango cha lami. (Makofi)