Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kabula Enock Shitobela

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza:- Je, lini Serikali itaongeza wataalam wa afya katika Hospitali ya Bugando na Sekou Toure kwa kuwa kuna upungufu mkubwa?

Supplementary Question 1

MHE. KABULA E. SHITOBELA: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali bado kuna upungufu hasa kwa wagonjwa wa saratani; lini sasa Serikali itatuongezea wataalam zaidi katika hospitali hizo mbili za Sekou Toure na Bungando hasa wataalam wa saratani? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri ambayo ameifanya kwa sekta ya afya kwa kipindi hiki chote alichokuwepo Bungeni, lakini nimwambie ni kweli kwenye Idara ya Kansa ambayo Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenye eneo hilo kwa hospitali tu ya Bugando amewekeza shilingi bilioni 12 na vifaa na sasa rufaa za kutoka Bugando kwenda Ocean Road zimepungua, wanaoenda Ocean Road ni chini ya asilimia moja, maana yake sasa watu wengi wanabaki kule Kanda ya Ziwa kwa ajili ya uwekezaji uliopo.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge katika nafasi 144 ambazo zimepangwa hapa tutafikiria zaidi na tutaelekeza kwenye maeneo yale ambayo yana mapungufu kama hilo eneo ambalo umelisema la kansa.

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Primary Question

MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza:- Je, lini Serikali itaongeza wataalam wa afya katika Hospitali ya Bugando na Sekou Toure kwa kuwa kuna upungufu mkubwa?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Spika, ahsante, Manispaa ya Ilemela ina upungufu wa wauguzi 111 kati ya 205 wanaotakiwa; wa teknolojia 33 kati ya 40 wanaotakiwa pamoja na wataalam wa dawa 11 kati ya 34 wanaotakiwa; je, ni lini manispaa hii itapata wataalam hawa ili waweze kufanya kazi yake vizuri ukizingatia tuna hospitali ya wilaya sasa?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kweli kuna upungufu maeneo mbalimbali hasa inatokana na upungufu halisi, lakini ni kwa sababu wakati mwingine wamesema hospitali ya wilaya inahitaji kiasi hiki, hospitali ya mkoa inahitaji kiasi hiki bila kuangalia load yaani namba ya wagonjwa. Nakubalina na wewe kwa Mwanza inawezekana ikawa ni kweli kwa sababu ni mjini na kuna watu wengi upungufu huo ukawepo, lakini nikuhakikishie tu katika ajira ambazo zinapangwa sasa tunatakiwa kwenda kuangalia siyo tu kuangalia hii ni hospitali ya wilaya, hiki ni kituo cha afya hii ni nini tunaenda kuangali je, hawa watu kwa siku wanahudumia wagonjwa wangapi? Wagonjwa ni wangapi wanaolazwa halafu tunaamua kupeleka kwa sababu tumekuja kugundua kuna vituo vya afya vinatibu wagonjwa wengi kwa siku kuliko hata hospitali ya wilaya.

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza:- Je, lini Serikali itaongeza wataalam wa afya katika Hospitali ya Bugando na Sekou Toure kwa kuwa kuna upungufu mkubwa?

Supplementary Question 3

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Waziri, niishukuru Serikali; Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara imejengwa katika Jimbo letu la Babati Mjini na wataalam hao wamekuwa wakifanya vizuri kuwahudumia wananchi wetu, lakini tatizo kubwa linalolalamikiwa ni gharama kubwa ya matitabu ni gharama kubwa sana. Je, Serikali ipo tayari kwenda kuchunguza ni kwa nini matibabu haya yamekuwa yakilalamikiwa na wananchi? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimesema jana, kwa kweli kwenye hospitali zetu za mikoa gharama za matibabu siyo kubwa kiasi hicho, lakini specifically Mheshimiwa Mbunge ninaomba mimi na wewe wiki ijayo ikiwezekana tukapitia pale tuone specifically kwa maana ya hospitali yako ya Mkoa wa Manyara ni nini walichokikosea kwenye formula ya kupanga bei mpaka sasa tufikie mahali ambapo watu wanalalamika kwamba bei ni ghali. (Makofi)

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. KABULA E. SHITOBELA aliuliza:- Je, lini Serikali itaongeza wataalam wa afya katika Hospitali ya Bugando na Sekou Toure kwa kuwa kuna upungufu mkubwa?

Supplementary Question 4

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi nami ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Mtakatifu Benedict ya Ndanda Mission ndiyo hospitali pekee kwenye Mkoa wa Mtwara na Lindi inayotoa huduma za kansa. Hata hivyo wana upungufu wa vifaa pamoja na wataalam; je, Serikali haioni haja ya kuwashika mkono ili waweze kutoa huduma hizo kwa uhakika wa kupunguza foleni ya watu wanaosafirishwa kuja Dar es Salaam kwa maana ya Muhimbili pamoja na Ocean Road? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza ni kwamba tuna Hospitali ya Kanda ambayo iko Mtwara kwa maana ya ukanda huo ambayo Serikali imefanya uwekezaji mkubwa sana na pale sasa hivi kuna ujenzi mkubwa sana wa ghala la kuweka dawa na vitu vingine.

Mheshimiwa Spika, pia kwenye hiyo hospitali ambayo sasa unaisema Mheshimiwa Mbunge ninakuomba tupitie mikataba yake na Serikali kwamba inasemaje na makubaliano yalikuwa nini, ni maeneo gani ambayo tulitakiwa tushirikiane, baada ya kujua hilo basi tushirikiane kwa mwongozo wa Mheshimiwa Waziri wa Afya ili tuweze kuona ni namna gani tunaweza kwenda.

SPIKA: Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri.

Mheshimiwa Spika, wakati tukiendelea na majibu ya Mheshimiwa Waziri ya kufuatilia mikataba na vitu vingine, lakini tunayo njia nyepesi ya mkato ambayo tunaweza kuanza nayo na nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kupitia Wizara tutashirikiana na Menejimenti ya Hospitali, tutengeneze mpango mkakati wa outreach program tupeleke madaktari wetu bingwa kutoka Ocean Road wakaone ni namna gani haraka sana ikiwezekana mwezi wa saba ama wa nane wanaweza kukutana na wataalam wetu pale na wakaweka kambi ya kuanza kufuatilia namna nzuri ya kuweza kuondoa tatizo hilo la matibabu ya kansa hapa. (Makofi)