Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Ester Edwin Malleko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha miundombinu ya Masoko ya Mwika na Makuyuni?
Supplementary Question 1
MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa Serikali imeahidi kwamba itajenga soko jipya kwa eneo la Makuyuni; je, ni lini sasa mchakato wa kumpata mzabuni utakamilika ili soko hilo lianze kujengwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika eneo la Mwika kumekuwa na msongamano mkubwa sana na inapelekea wakati mwingine wafanyabiashara kupata ajali kutokana na kwamba wanafanya biashara zao barabarani. Ni lini sasa Serikali itatoa fedha hizo na ziweze kwenda kununua eneo ambalo hawa
wananchi wanaweza kupata huduma hiyo kwa usahihi zaidi? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nimpongeze sana Mheshimiwa Esther Edwin Malleko, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Kilimanjaro, kwa uchapakazi wake na amekuwa mfuatiliaji sana. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Moshi Mjini na Moshi Vijijini kwamba Serikali inatambua sana umuhimu wa masoko haya mawili; Soko la Makuyuni kwa ajili ya kuhakikisha kwamba tunaboresha mazingira ya biashara kwa wananchi na
tayari tumeshakubaliana na Wizara ya Kilimo na tumeshaandaa hati pacha ambayo itamilikiwa na halmashauri na Wizara ya Kilimo na tuko hatua za mwisho kukabidhi hati pacha hii ya Wizara ya Kilimo ili Wizara ya Kilimo iweze kupata mkandarasi kwa ajili ya
ujenzi wa Soko la Makuyuni. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tuko hatua nzuri sana ya kuhakikisha kwamba tunajenga soko hilo na kuboresha mazingira ya biashara kwa wananchi wa Makuyuni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kuhusiana na Soko la Mwika tunatambua kwamba soko lile ni dogo na linapelekea wafanyabiashara kupanga bidhaa zao barabarani jambo ambalo ni hatarishi na ndio maana tumekwishatenga shilingi 70,000,000 katika mwaka wa fedha ujao 2026/2027 tunaoanza Julai hii, ili tuweze kununua eneo lenye ukubwa wa ekari moja na kujenga soko ambalo litaondoa adha ya wafanyabiashara
kubanana na kupanga bidhaa barabarani. (Makofi)
Name
Asha Juma Feruz
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha miundombinu ya Masoko ya Mwika na Makuyuni?
Supplementary Question 2
MHE. ASHA J. FERUZ: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi, nami ninaomba nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri swali langu la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini sasa Serikali itaboresha
miundombinu katika soko la mazao lililoko katika Kata ya Somangila na Pembamnazi katika Wilaya ya Kigamboni?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Asha, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Dar es Salaam kwamba yako masoko likiwemo Soko la Somangila
ambalo linahitaji kuboreshwa na tayari Serikali tumeweka mkakati wa muda mfupi, wa muda wa kati na muda mrefu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, kwa kushirikiana na
halmashauri kutenga mapato ya ndani kuendelea kuboresha masoko hayo, lakini pili kwa kuandaa miradi ya kimkakati kwa ajili ya kujenga masoko mahususi katika maeneo ambayo tunahitaji kuboresha masoko hayo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa Soko la Somangila ni miongoni mwa masoko ambayo tutayapa kipaumbele katika mipango yetu ili tuweze kuliboresha. (Makofi)
Name
Edward Olelekaita Kisau
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kiteto
Primary Question
MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha miundombinu ya Masoko ya Mwika na Makuyuni?
Supplementary Question 3
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti,
ninakushukuru kwa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Soko la Mji wetu wa Kibaya ni la muda mrefu kidogo wafanyabiashara wanahangaika kila wakati na mapato ya halmashauri ni madogo sana. Sasa lini Serikali itatuletea angalau shilingi 1,000,000,000 tu ili tuweze kufumua lile soko letu la Kibaya?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mji wa Kibaya ni miongoni mwa miji mikongwe sana katika nchi yetu na katika Jimbo la Kiteto kwa Mheshimiwa Edward Olelekaita na ni mara kadhaa Mheshimiwa Mbunge
amefuatilia kuhusiana na uboreshaji wa soko hilo. Mimi
nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua umuhimu wa kuboresha Soko la Kibaya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, na nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI nimwelekeze Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kiteto waandae andiko la kimkakati kutokana na umuhimu wa Soko la Kibaya wawasilishe Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI ili tuweze kufanya taratibu kwa awamu kuona uwezekano wa kuboresha soko hilo. (Makofi)
Name
Fagason Aron Nkingwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbogwe
Primary Question
MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha miundombinu ya Masoko ya Mwika na Makuyuni?
Supplementary Question 4
MHE. FAGASON A. NKINGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi hii nami niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo langu la Mbongwe ambalo ni Halmashauri ya Mbongwe haina soko kabisa na kwa sababu hiyo Halmashauri ya Mbongwe iko pale Kasosobe, lakini pale Mbongwe hakuna soko hata la uuzaji wa nyanya na kwa sababu taasisi zote za Serikali ziko pale. Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha inaenda kujenga soko kubwa pale kwenye Halmashauri ya Mbongwe? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, Serikali ilishatoa maelekezo na ndiyo msimamo wa Serikali kwamba maeneo yote ya halmashauri ambayo ni muhimu kwa huduma za kijamii yakiwemo masoko ni
kipaumbele katika mipango ya halmashauri na kwa kuwa Mbunge wa Mbongwe, Mheshimiwa Fagason anasema Halmashauri ya Mbongwe haina soko kabisa, ninaomba nitumie nafasi hii kumsisitiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbongwe kupitia Baraza lake la Madiwani wakae waainishe eneo kwa ajili ya kujenga soko katika Halmashauri ya Mbongwe, waanze kutenga fedha kwenye mapato ya ndani na ikibidi wawasilishe maombi ili Serikali iweze kuwaunga mkono, lakini dhamira ni kuhakikisha kwamba Halmashauri ya Mbongwe inapata soko zuri ambalo litahudumia wananchi katika eneo hilo. (Makofi)
Name
Alan Thomas Mvano
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kakonko
Primary Question
MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha miundombinu ya Masoko ya Mwika na Makuyuni?
Supplementary Question 5
MHE. ALAN T. MVANO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimesimama hapa kushukuru sana Serikali yetu hii inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa tuliwasilisha ombi la fedha kwa ajili wa soko na tumepokea fedha na ujenzi unaendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu ni moja tu, Mheshimiwa Naibu Waziri kama atakuwa tayari twende pamoja Kakonko aangalie maendeleo ya ujenzi na kuhakikisha kwamba sasa ujenzi unakamilika mapema ili kuwanufaisha wananchi wa Kakonko? Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nimpongeze sana Mheshimiwa Alan Mvano, Mbunge wa Jimbo la Kakonko kwa ufuatiliaji wake wa mara kwa mara na nipokee pongezi ambazo amempa Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na ni hakika kwamba, Mheshimiwa Rais amefanya kazi kubwa sana ya kuboresha miundombinu ya masoko katika halmashauri zetu.
(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba niko tayari tutapanga ili tuone baada ya kumaliza Bunge letu hili tuweze kufika katika Jimbo la Kakonko, tukague miradi ya maendeleo, lakini pia kuona hatua za ujenzi wa soko hilo. (Makofi)
Name
Charles Mhando Njama
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Korogwe Mjini
Primary Question
MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha miundombinu ya Masoko ya Mwika na Makuyuni?
Supplementary Question 6
MHE. CHARLES M. NJAMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya soko letu la Manundu katika Jimbo la Korogwe Mjini ni mbaya sana na katika kipindi cha mvua zilizopita wafanyabiashara wamepata hasara kubwa kwa sababu ya mafuriko kwa sababu ya miundombinu ambayo imechakaa katika soko lile na kuna hatari kubwa ya kupata hatari ya moto ikitokea basi hasara itakuwa kubwa zaidi. Je, ni lini Serikali itakuwa tayari kwenda kufanya ukarabati na maboresho ya soko lile ili kuendana na hali ya maendeleo ya Mji wa Korogwe Mjini? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na nimpongeze Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini, lakini nirejee kuwasisitiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwamba miundombinu ya masoko kwanza ni sehemu muhimu ya huduma kwa jamii, lakini pili, ni sehemu muhimu ya vyanzo vya mapato na nina hakika halmashauri inakusanya mapato katika soko hilo katika Halmashauri ya Korogwe Mjini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni wajibu wa halmashauri kutenga fedha kupitia mapato ya ndani, kufanya matengenezo kuhakikisha soko lile linahuduma muhimu kama maji, vyoo barabara ya kuingia na kutokea kwa kushirikiana na TARURA. Kwa hiyo, nimwelekeze Mkurugenzi watekeleze ukarabati wa
soko hilo mapema iwezekanavyo, lakini na sisi Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI tutafuatilia kuona kwamba soko hilo limekarabatiwa. (Makofi)