Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Michael Constantino Mwakamo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibaha Vijijini
Primary Question
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO aliuliza: - Je, Serikali imejipangaje kutatua migogoro ya ardhi kati ya Wananchi na Wawekezaji wenye mashamba makubwa Kibaha Vijijini?
Supplementary Question 1
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwanza niikumbushe Serikali kwamba, kuna eneo la Soga kwenye shamba la Mohamed Enterprise tayari kulishakuwa na maelekezo ya ekari 500 kurudi Serikalini. Kwa kuwa, kuna changamoto mbalimbali zinazoendelea kusababisha kutokutekelezwa kwa agizo hilo.
Je, Waziri atakuwa yupo tayari kuambatana nami mara baada ya Bunge kwenda kusaidia kuondoa hizo changamoto zinazosababisha utekelezaji wa agizo hilo? (Makofi)
Mheshimiwa  Spika,  swali  langu  la  pili,  pale  Kata  ya  Kikongo  kuna mwekezaji anaitwa Trans-continental na shamba moja la UFC ambalo lipo mikononi  mwa  Serikali,  kuna  wananchi  ambao  wapo  pale  muda  mrefu, wana miaka mingi, karibu 15 mpaka 20, na wawekezaji hao hawajaendelea.
Je, Serikali inatoa tamko gani kuwaruhusu wawekezaji hao kuendelea na shughuli zao? (Makofi)
 
											Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
								NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Michael Costantino Mwakamo, Mbunge wa Kibaha Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwanza kuhusiana na suala la Soga kwenye shamba la Mohamed Enterprise naafikiana nawe Mheshimiwa Mbunge kwamba tutakwenda kutatua kero hizi maana tunaambiwa yanayoendelea huko siyo mazuri sana.
Mheshimiwa Spika, jambo la pili kuhusiana na jambo la  trans- continental kule Kikongo na  Waya mifugo, Mheshimiwa Mbunge nataka nikuhakikishie utayari wa Serikali, kwenda kushirikiana nawe kutatua kero hizi. Pili, katika Shamba la Waya, tutashirikiana na Wizara ya Mifugo kuhakikisha kwamba hatua zinazostahiki kufuatwa ili kukabidhiwa shamba hilo kama ambavyo Serikali iliamua nazo pia zinafuatwa. (Makofi)
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved