Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
 
											Name
Deodatus Philip Mwanyika
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Njombe Mjini
Primary Question
MHE. SALIM MUSSA OMAR aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza magari ya kisasa ya zimamoto?
Supplementary Question 1
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru saba kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa mikoa ambayo inategemea sana uchumi wa misitu; mikoa ya nyanda za juu Kusini na hasa Mkoa wa Njombe, wananchi wamepata umasikini mkubwa sana kutokana na moto ambao unatokea mwaka baada ya mwaka. Serikali ina mpango gani wa kuwa na mkakati wa kusaidia kwa kuleta vifaa vya kisasa kwenye maeneo hayo ambayo yanashambuliwa sana na moto?
 
											Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
								NAIBU WAZIRI	WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Deo Mwanyika kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli anayoyasema hutokea kwenye mikoa na wilaya nyingi zenye misitu. Kwa kutambua hilo ndiyo maana Mkoa wa Njombe hadi sasa wanayo magari mawili, moja liko Njombe Mjini na lingine liko Makambako. Ni dhamira ya Serikali  kadiri  uwezo  wetu utakavyoongezeka wa kununua magari ya kuzimia moto, Mkoa wa Njombe pia utazingatiwa.
							
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved