Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 50 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 637 | 2025-06-20 |
Name
Kenneth Ernest Nollo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bahi
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA K.n.y. MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya Kata ya Mpalanga – Bahi?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Mpalanga ina vijiji vitatu ambavyo ni Mpalanga, Nholi na Chidilo na ina jumla ya watu 13,664 kwa Sensa ya Watu na Makazi ya m
waka 2022. Aidha, vijiji viwili vya Mpalanga na Chidilo vina zahati na Kijiji cha Nholi ujenzi wa zahanati unaendelea. Aidha, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali ilipeleka shilingi milioni 60 kwa ajili ya ukamilishaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa huduma za rufaa na upasuaji wa dharura zinazotokea katika Zahanati za Kata ya Mpalanga zinahudumiwa na Kituo cha Afya Chipanga.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika Kata za kimkakati zitakazokidhi vigezo kote nchini. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved