Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 50 Enviroment Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano 638 2025-06-20

Name

Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASYA MWADINI MOHAMMED K.n.y. MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza:-

Je, Serikali ina Mikakati gani ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Nchini? (Makofi)

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inashirikiana kikamilifu na Jumuiya za Kimataifa katika kubuni mikakati na hatua madhubuti za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika ngazi zote. Baadhi ya Mikakati inayochukuliwa na nchi katika kukabiliana na athari hizo ni pamoja na kuridhia Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Itifaki ya Kyoto ya makubaliano ya Paris, kuandaa na kutekeleza nyenzo za kisera zitakazosaidia kutoa dira na kuibua programu na kutekeleza miradi inayosaidia jamii katika maeneo mbalimbali ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi, hii inajumuisha mikakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (2021), Mpango Kabambe wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022-2032) na Mchango wa Taifa katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (2021).

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo mbalimbali nchini. Miradi hii inajumuisha upandaji wa miti, usambazaji wa majisafi kwa matumizi ya majumbani na mifugo, ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji, matumizi ya nishati mbadala ikiwemo nishati safi ya kupikia ili kupunguza kasi ya ukataji wa misitu, ujenzi wa kuta katika maeneo ya fukwe za bahari yanayokabiliwa na mmomonyoko wa ardhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali itaendelea na ujenzi wa matuta na mabwawa kudhibiti mafuriko, kuwezesha jamii kubuni miradi mbadala ya kuongeza kipato na iliyo rafiki kwa mazingira na kurejesha maeneo ya ardhi yaliyoharibika.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru. (Makofi)