Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asya Mwadini Mohammed

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASYA MWADINI MOHAMMED K.n.y. MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza:- Je, Serikali ina Mikakati gani ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Nchini? (Makofi)

Supplementary Question 1

MHE. ASYA MWADINI MOHAMMED: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana, nina maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na jitihada za Serikali za kuhamasisha masuala mazima ya upandaji miti mashuleni ambao wana kampeni ambayo inasema, “Soma na Mti,” lakini kumekuwa na changamoto kubwa ya wananchi nje ya mashule, bado kupata taaluma hii ya suala la upandaji wa miti. Miti imekuwa inakatwa sana kiholela na kusababisha masuala mbalimbali ya mabadiliko ya tabianchi. Je, ni nini mkakati wa Serikali kuja na kampeni maalum kwa jamii na kuhamasisha suala zima la upandaji wa miti? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kumekuwepo na uchafuzi mkubwa wa masuala ya fukwe zetu. Kuna baadhi ya hoteli wawekezaji ndani ya nchi yetu na wanaokuja, wanajenga chini ya kingo za mito, na wengine wanapewa vibali hadi kuchimba bahari. Hii inasababisha pia mabadiliko ya tabianchi, maji kuzidi kwenye kima ya bahari na kuwafikia wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni nini mkakati wa Serikali juu ya kutoa elimu ama kwenda nao hawa wawekezaji kuja na mpango maalumu wa kuhakikisha fukwe zetu na kingo zinahifadhiwa kwa utulivu? Ahsante. (Makofi)

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba tumefanya kasi kubwa ya kuhakikisha kwamba tunaendelea kuelimisha wananchi juu ya suala zima la upandaji na ushughulikiaji wa miti. Moja ya miongoni mwa hatua hiyo ilikuwa ni kuanzisha Kampeni Maalum ya ‘Kusoma na Mti’ ambapo tuliwataka wanafunzi wote wa shule za msingi, sekondari, vyuo na vyuo vikuu kuhakikisha kwamba wanapanda miti ya kutosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hayo, tumeendelea kutoa elimu shuleni, kwenye semina tofauti na hata kwenye makongamano yetu yanayohusiana na masuala ya mazingira, tumekuwa tukielimisha watu suala zima la kupanda miti. Kikubwa zaidi tunaendelea kutoa elimu kwenye matukio makubwa ya Kitaifa, hata matukio ya kila siku ambayo tunayafanya katika jamii kusudi tuongeze speed ya upandaji miti na kuokoa mazingira.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na changamoto ya kuchimbwa bahari na kutokuhifadhi fukwe, ni kweli zipo shughuli zinafanyika karibu na maeneo haya ya ufukwe zikiwemo za ujenzi wa hoteli, ukataji wa miti hasa mikoko na vitu vingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuhakikisha kwamba tunaendelea kuwaelimisha wananchi, ni kwamba tunawaomba sana wananchi Tanzania nzima waendelee kutunza fukwe na maeneo ya Bahari, lakini kubwa wazingatie ule mwongozo wetu wa mita 60, kwamba shughuli zote zinazofanyika karibu na vyanzo vya maji ikiwemo bahari, mito, maziwa na vyanzo vingine zihakikishe kwamba zinazingatia mwongozo wa mita 60. Ninakushukuru. (Makofi)