Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 50 Enviroment Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano 639 2025-06-20

Name

Bernadeta Kasabago Mushashu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. BERNADETHA K. MUSHASHU aliuliza: -

Je, biashara ya kununua na kuuza carbon imeinufaishaje Tanzania?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuratibu na kuimarisha usimamizi wa biashara ya kaboni nchini ambapo jumla ya miradi 73 ya biashara ya kaboni imeshasajiliwa na ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Miradi hiyo ni ya sekta za misitu 51%, nishati 33%, taka asilimia tatu, kilimo asilimia nane na mifugo asilimia tano.

Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji wa miradi hii huchangia katika uhifadhi na urejeshaji wa misitu na ardhi ili kuongeza fursa za ajira na pato la wananchi kwa ujumla na kupunguza uzalishaji wa gesijoto ambapo huchangia katika kufikia malengo ya utekelezaji wa mchango wa Taifa katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi (Nationally Determined Contribution).

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, biashara ya kaboni imeanza kuleta manufaa ya kiuchumi katika baadhi ya maeneo nchini ambapo kiasi cha shilingi bilioni 45 zimelipwa na kunufaisha wananchi katika Halmashauri 10 nchini kama gawio la mauzo ya viwango vya kaboni. Fedha hizi hutumika katika kutekeleza miradi ya kijamii katika vijiji husika kama vile ujenzi wa shule, zahanati, malipo ya bima za afya, ada za shule na chakula kwa wanafunzi. Ninakushukuru. (Makofi)