Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Bernadeta Kasabago Mushashu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BERNADETHA K. MUSHASHU aliuliza: - Je, biashara ya kununua na kuuza carbon imeinufaishaje Tanzania?
Supplementary Question 1
MHE. BERNADETHA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Ili uweze kufanya hii biashara ya kuuza na kununua kaboni, ni vigezo gani vinavyotakiwa?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa Mkoa wa Kagera una mvua nyingi, na kwa sababu ya mvua hizo tuna miti na misitu mingi, kwa sababu inaonekana hii biashara ya kuuza na kununua kaboni ni biashara nzuri, ina manufaa makubwa kwa Taifa, lakini inaweza ikamnufaisha hata yule anayefanya hii biashara. Je, ni lini sasa Serikali itaenda mkoani Kagera kuhamasisha ili kusudi hawa watu nao waanze hii biashara waweze kunufaika? (Makofi)
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii nimpongeze sana Mheshimiwa Mushashu kwa kuwa amekuwa mdau mzuri wa mazingira hasa kwenye masuala haya ya kaboni. Ili tuweze kukusajili, ama uweze kusajiliwa na kuweza kufanya shughuli hizi za biashara ya kaboni, vipo vigezo ambavyo hivyo lazima vifikiwe ndipo tuweze kumpatia mtu fursa hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, tuhakikishe kwamba amepata eneo ambalo litakuwa linaweza likafanyiwa hiyo biashara. Pia, tuhakikishe kwamba awe na kampuni ambayo imesajiliwa, awasilishe andiko maalum kwenye kituo chetu cha kaboni pale Morogoro, andiko ambalo litatushawishi ama litashawishi taasisi inayosimamia kaboni kuweza kumpatia fursa kuweza kufanya hiyo biashara na ahakikishe kwamba amelipa fee ya usajili.
Mheshimiwa Naibu Spika, kikubwa zaidi ahakikishe kwamba awe mzalendo wa kuhakikisha yupo tayari kufanya shughuli hizi bila ya kuathiri mazingira mengine ambayo yamezunguka wanakijiji wa maeneo hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, kikubwa nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mkoa huo aliouzungumza, tayari elimu imeshaanza, tumeshafika huko. Kikubwa, tunaendelea kufanya bidii ya kuhakikisha kwamba tunatoa elimu kwa wananchi sambamba na kuwaeleza faida, fursa na changamoto mbalimbali ambazo zinapatikana katika biashara hii. Ninakushukuru. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved