Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 50 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 640 2025-06-20

Name

Masache Njelu Kasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lupa

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: -

Je, lini Serikali itafanya juhudi za makusudi kupeleka umeme kwenye maeneo ya Wachimbaji Wadogo Wilayani Chunya?

Name

Doto Mashaka Biteko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukombe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini inatekeleza mradi wa kupeleka umeme katika migodi midogo nchini ambapo katika Wilaya ya Chunya, Serikali imepeleka umeme katika maeneo ya migodi ya wachimbaji wadogo 16 kati ya migodi 18 iliyopo Wilayani hapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa maeneo mawili ya migodi yaliyobaki, Mkandarasi aitwaye OK Electrical and Electronics anaendelea na kazi, na anatarajia kukamilisha kupeleka umeme hivi karibuni.