Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya juhudi za makusudi kupeleka umeme kwenye maeneo ya Wachimbaji Wadogo Wilayani Chunya?

Supplementary Question 1

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali kwa kufikisha umeme kwenye haya maeneo 16 kati ya maeneo 18. Kwa niaba ya Mbunge wa Chunya (Mheshimiwa Njelu Kasaka), anaipongeza Serikali, pia na Mheshimiwa Waziri Mkuu juzi alikuwa kule kwa ajili ya kufungua Kiwanda cha Kuchenjua shaba ambacho kwa kweli kinategemea sana umeme. Pia tuna maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza. Kumekuwa na changamoto ya umeme Chunya kwamba una nguvu ndogo kutokana na matumizi makubwa ya ile line. Ni lini Serikali itajenga sub-station kwa ajili ya kuongezea nguvu ili umeme huu uweze kuwafikia Wanachunya na wenye migodi hii ili wapate umeme wa uhakika wakati wa shughuli zao za uchimbaji?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili. Ni kwa ajili ya wananchi wa Jimbo la Makete ambalo mimi ni Mbunge wao. Ninaomba kuuliza kwamba, sisi watu wa Makete tulikuwa na changamoto ya umeme kutokea Mbeya kwenda Makete na sasa Serikali imetubadilishia kutoka Makete kwenda Njombe.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto ambayo tunaipata, umeme ni wa uhakika, lakini kumekuwa na kukatikakatika kwa umeme mara kwa mara. Tunahitaji kitu kimoja kinaitwa Automatic Power Regulator ambapo huwa vinafungwa na Wizara. Ni lini vifaa hivyo vitafungwa ili umeme Makete usikatike?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Sanga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Chunya ni eneo ambalo lina utajiri mkubwa wa madini, na kutokana na hili ndiyo maana tumeelekeza nguvu ya kupeleka mradi wa gridi imara kule, lakini kasi ya kugundua madini ni kubwa sana. Hivi tunavyozungumza, tayari kuna maeneo mapya 29 wananchi wamegundua dhahabu. Kwa hiyo, kama Serikali, tumeona umuhimu wa kuongeza nguvu katika eneo lile. Kwa hiyo, kupitia gridi imara, tunaenda kujenga sub-station nyingine kubwa kwa ajili ya kuongeza uwezo kwenye eneo lile.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na swali lake la pili, ambapo anasema kwamba kwa Makete umeme una-fluctuate, na kwamba kuna kifaa ambacho kinahitajika kuwekwa. Ninaomba nimhakikishie, baada ya hapa tukutane, tuzungumze, ili tuone mahitaji halisi ni yapi, halafu tuweze kuelekeza wataalamu wetu. (Makofi)

Name

Jesca Jonathani Msambatavangu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: - Je, lini Serikali itafanya juhudi za makusudi kupeleka umeme kwenye maeneo ya Wachimbaji Wadogo Wilayani Chunya?

Supplementary Question 2

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo hilo hilo la umeme ku-fluctuate linatokea katika eneo la Mipango na Miyuji kule. Je, kuna mpango gani wa kurekebisha kwa maana ni katikati ya Jiji?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo hili liko kwenye maeneo mengi nchini. Kama mnavyokumbuka, Serikali iliwasilisha taarifa hapa kwamba, moja ya changamoto kubwa ni mifumo yetu ya kusambaza umeme ambayo imechakaa na kwamba tumekuja na utaratibu huu wa kuwa na mradi wa gridi imara ili kuondoa mifumo ya zamani na kuleta mifumo mipya. Kazi hii itachukua muda kidogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninawaomba Waheshimiwa Wabunge wawe na Subira, kwani tukiweza kukamilisha jambo hili, basi tatizo hili la fluctuation litakuwa limeondoka.