Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 50 Energy and Minerals Wizara ya Madini 641 2025-06-20

Name

Lucy John Sabu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CHARLES M. KAJEGE K.n.y. MHE. LUCY J. SABU aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwa na Sera rafiki ya nishati ya umeme kwa Vijana wanaojihusisha na Uzalishaji kwenye Viwanda vidogo vidogo?

Name

Doto Mashaka Biteko

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukombe

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Sera ya Taifa ya Nishati ya Mwaka 2015, imelenga kuwezesha upatikanaji wa Nishati ya Umeme nchini kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya kiuchumi pamoja na kijamii kwa watu wote wakiwemo vijana.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kutekeleza sera hii, Serikali kupitia REA, imekamilisha kupeleka umeme katika vijiji vyote vya Tanzania Bara na sasa kazi ya kusambaza umeme katika vitongoji inaendelea. Aidha, REA inaendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi wakiwemo vijana kuhusu matumizi ya umeme kwenye uzalishaji mali hususan viwanda vidogo vidogo.