Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Charles Muguta Kajege
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwibara
Primary Question
MHE. CHARLES M. KAJEGE K.n.y. MHE. LUCY J. SABU aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwa na Sera rafiki ya nishati ya umeme kwa Vijana wanaojihusisha na Uzalishaji kwenye Viwanda vidogo vidogo?
Supplementary Question 1
MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri, lakini nina swali dogo. Wakati wa ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu Jimboni Mwibara, aliahidi kuwa Serikali itaweka umeme wa solar katika Kisiwa cha Nafuba. Je, ni lini ahadi hiyo itatekelezwa?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Kajege kwamba ahadi zote za viongozi wetu wakuu ni maelekezo, na Serikali itahakikisha inatekeleza ahadi ile.
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CHARLES M. KAJEGE K.n.y. MHE. LUCY J. SABU aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kuwa na Sera rafiki ya nishati ya umeme kwa Vijana wanaojihusisha na Uzalishaji kwenye Viwanda vidogo vidogo?
Supplementary Question 2
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru. Gharama za uendeshaji na hasa viwandani imekuwa ni kubwa sana na zaidi ikichangiwa na gharama kubwa ya umeme. Sasa ili kuweza kuhakikisha kwamba tuna viwanda vingi nchini hasa hivi vidogo vidogo ambavyo vimeelekezwa kwenye swali la msingi, Serikali haioni kwamba kuna haja sasa ya kupitia upya gharama hizi za umeme viwandani ili kuwawezesha Watanzania wengi kuwekeza kwenye viwanda vidogo vidogo?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya mikakati ya Serikali ya kuhakikisha kwamba inadhibiti upandaji wa gharama za uzalishaji ni kuwa na utaratibu wa kufanya review ya viwango vyetu hivi mara kwa mara. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Matiko, jambo analolizungumza ni jambo ambalo ndani ya Serikali sasa hivi linafanyika.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved