Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 50 Water and Irrigation Wizara ya Maji 642 2025-06-20

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE K.n.y. MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza kujenga mradi wa maji wa Kyerwa, Nyakatuntu na Kamuli – Kyerwa?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026 imepanga kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wa kimkakati katika Wilaya ya Kyerwa Mkoa wa Kagera. Kazi zinazotarajiwa kufanyika kupitia mradi huo ni pamoja na ujenzi wa chanzo cha maji katika Mto Kagera, ujenzi wa matanki yenye jumla ya ujazo wa lita 3,300,000, ulazaji wa bomba mbalimbali zenye urefu wa kilometa 225, sanjari na ujenzi wa vituo 75 vya kuchotea maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miezi 18 ambapo unalenga kunufaisha zaidi ya wananchi 168,670 waishio kwenye vijiji 37 vilivyopo kwenye Kata Saba za Kyerwa, Nyakatuntu, Nyaruzumbura, Kitwe, Businde, Bugala, na Kamuli, ninakushukuru.