Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Atupele Fredy Mwakibete

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busokelo

Primary Question

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE K.n.y. MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza kujenga mradi wa maji wa Kyerwa, Nyakatuntu na Kamuli – Kyerwa?

Supplementary Question 1

MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali kwa niaba ya Mheshimiwa Innocent Sebba Bilakwate, ninauliza maswali mawili ya nyongeza. Mradi huu Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kyerwa ameuzungumza kwa zaidi ya miaka miwili hapa Bungeni, mimi nikiwa shahidi, na sasa Serikali inasema inakwenda kutekeleza kwa mwaka ujao wa fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba commitment ya Serikali, kwamba ni kweli utekelezwa mwaka ujao wa fedha, ukizingatia kwamba miaka miwili yote majibu ya Serikali ilikuwa ni kwamba imepangwa kwenye bajeti na huwa haitekelezeki?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Wananchi wa Jimbo la Busokelo tumekuwa na miradi zaidi ya mitano inayotekelezeka ndani ya lile Jimbo, lakini kwa muda mrefu haijakamilika. Ni lini Serikali inakwenda kukamilisha miradi hii hususan katika Kata za Luteba, Segese, Kandete, Mpombo, pamoja na Lwangwa? Ahsante.

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mwakibete, nimwambie kwamba, katika bajeti ya mwaka 2025/2026 ambayo imepitishwa juzi, Waheshimiwa Wabunge wameiridhia, na jumla ya shilingi trilioni 1.06 ziliidhinishwa hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwambie tu Mheshimiwa kwamba, miradi yote ambayo ilikuwa labda inasuasua kwa namna moja ama nyingine, inakwenda kukamilishwa kwa wakati ili iweze kunufaisha, kwa maana kwamba wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwambie Mheshimiwa Mbunge, na hiyo ndiyo commitment ya Serikali, kwamba miradi yote fedha hizi ambazo Wabunge wameziidhinisha ndizo zitakwenda kukamilisha miradi yote ambayo ipo katika Jimbo hilo la Busokelo na maeneo mengine yote, ahsante.